loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Adhabu ziongezwe kwa waamuzi watakaovurunda

IPO haja ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuiongeza adhabu kwa waamuzi ambao watavurunda katika mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pengine njia hii itasaidia kuongeza umakini wanapokuwa kazini.

Inafahamika kwamba TFF, wamefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa semina mbalimbali pamoja na mafunzo maalumu (Copa test) kabla ya msimu mpya kuanza lakini cha kushangaza mechi ya kwanza ya msimu madudu ya aibu uwanjani.

Mechi kati ya Ihefu na Simba ambayo ilichezwa Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda 2-1, mshika kibebendera namba mbili alionesha madhaifu makubwa kiasi cha kuvuruga ladha ya mchezo.

Mwamuzi huyo alikataa bao halali la Ihefu kabla ya kurudia kosa hilo kipindi cha pili alipokataa bao halali la Simba, ambalo limefungwa na Meddie Kagere, madai yake alikuwa ameotea.

Wakulaumiwa hapa siyo TFF, Bodi ya ligi wala Mwenyekiti wa Waamuzi Soud Abdi bali ni uzembe wa mwamuzi mwenyewe ambaye ameshindwa kusimamia sheria 17 zinazomuongoza katika mchezeshaji.

Nikweli sheria ya kuotea (off side), imekuwa ikiwachanganya waamuzi wengi lakini cha kustajaabisha makosa hayo yamejirudia mara mbili kwenye mchezo mmoja tena upande wake.

Sasa TFF na Bodi ya ligi ikumbukwe msimu uliopita iliingia lawamani sana kuhusu ubovu wa waamuzi na mara nyingi imekuwa ikiwakingia kifua kuwatetea wasishambuliwe na makocha au wachezaji.

Hiyo inaweza kuwa sawa lakini hakumalizi tatizo husika kitucha msingi hapo ni wao kuongeza ukubwa wa adhabu kwa yeyote atakayefanya kosa ambalo litakuwa lakizembe kama lile.

Adhabu ambayo itakwenda kuwa mfano kwa waamuzi wengine. Ligi ya Tanzania imekuwa maarufu sana pengine kutokana na ushindani uliopo pamoja na malipo mazuri kwa wachezaji uchezeshaji mzuri nao una nafasi yake katika kusaidia ligi kupiga hatua na kuwa maarufu zaidi.

Haipendezi kuona timu ndogo kama Ihefu ambayo ndiyo inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza inakwenda kukataliwa bao lake kirahisi kwa ukubwa wa Simba, pengine wenyewe walijipanga kupata angalau pointi moja lakini kukataliwa bao lao la kusawazisha kuliwavunja nguvu ya kucheza kwa uhuru Mataifa ya jirani pamoja na mdororo wa ligi zao lakini heshima kubwa imekuwa kwa waamuzi na ni mara chache sana kusikia timu au kocha akitoa lawama kwa mwamuzi, lakini tofauti na hapa kwetu.

Kila msimu waamuzi wa Tanzania wamekuwa wakitawala midomoni mwa makocha,viongozi na mashabiki wa timu hii inaeleza ukweli wa mapungufu waliyokuwa nayo kwani huko nyuma imewahi kuelezwa kwambi bingwa anayepatikana huwa anakuwa wa mipango na siyo juhudi binfsi za uwanjani.

TFF na Bodi ya ligi wanapaswa kufahamu kwamba, wapo watu wameweka pesa zao katika kusajili wachezaji kutoka nje, lakini pia yapo makampuni makubwa yamejitokeza kuzidhamini timu hizo wakitarajia kupata kitu kizuri sasa hiki cha juzi kama kitaendelea mpaka mwisho wa ligi ni makampuni mangapi yatajiondoa? Ndio maana Imepenya ikatoa ushauri wa bure kwa TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha wanatoa adhabu kali kwa waamuzi watakaovurunda kizembe ili waliobaki kuongeza umakini wanapokuwa kazini.

KWA sasa nchi nzima ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi