loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nchi za Ulaya zatakiwa kuondoa vizuizi

JUMUIYA ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific (OACPS) imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuondoa vizuizi vya kusafiri (travelbans) kwa baadhi ya nchi za OACPS hususan zile zilizoonesha kuwa salama zaidi dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona kama Tanzania. 

Wito huo ulitolewa katika kikao maalum cha mashauriano baina ya Jumuiya ya nchi za OACPS na nchi ya Ujerumani ambayo kwa sasa ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya.

Mashauriano hayo yaliyofanyika tarehe 9 Septemba2020 katika Ofisi za Jumuiya ya OACPS, Brussels nchini Ubelgiji, yaliongozwa naBalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja waUlaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za OACPS walioko Brussels,Mhe. Jestas Abuok Nyamanga na ujumbe wa Ujerumani uliongozwa na Waziri wa Masuala ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho laUjerumani, Dkt. Gerd MÙLLER.

Katika kikao hicho wajumbe walisisitiza umuhimu wa Umoja wa Ulaya kuendelea kuunga mkono Shirika la Afya Duniani (WHO) katikakusimamia ithibati za tafiti za chanjo za ugonjwa wa Corona na Shirika hilokuendelea kujengewa uwezo wa kusimamia utaratibu wa kuhakikisha kuwa chanjo itakayothibitika inawafikia mataifa yote kwa usawa na kwa gharama nafuu.

foto
Mwandishi: BRUSSELS

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi