loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Joto la uchaguzi mkuu lapanda

JOTO la uchaguzi mkuu wa utakaofanyika mwakani limeanza kupanda kutokana na vyama kuanza pilika pilika za kujiweka tayari kuhakikisha kinanyakua ushindi.

Wakati baadhi ya vyama vya upinzani maji yakiwafika shingoni na kuamua kukaa pembeni kutazama kinyang’anyiro hicho nje ya dimba, chama tawala kinaendelea na chaguzi za ndani za kuwachagua wagombea wa nafasi mbalimbali.

Chama kikuu cha upinzani kupitia mwenyekiti wake mwanasiasa mkongwe, Dk Kiza Besigye, kilitangaza mwezi uliopita kuwa hakitasimamisha mgombea katika uchaguzi huo.

Hatua ya chama hicho inatoa nafasi kwa mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kuchukua nafasi ya FDC.

Matukio mbalimbali yameanza kujitokeza yanayoonesha joto la kisiasa limepamba moto kuelekea uchaguzi huo.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Kazi, Mwesigwa Rukutana, alishikiliwa na polisi baada ya kudaiwa kumpiga risasi mfuasi wa mpinzani wake wakati wa upigaji kura za mchujo kuwania ubunge kupitia chama tawala NRM.

Kutokana na tukio hilo, Rais Yoweri Museveni alitoa mwito kwa wanasiasa kuwaheshimu wananchi na kuonya hakuna atakayevumiliwa kwa kuchochea machafuko ya kisiasa nchini Uganda.

foto
Mwandishi: KAMPALA ,UGANDA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi