loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaribio ya chanjo ya covid-19 kuanza

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imethibitisha kuwa, Kenya ipo katika hatua za mwisho za kuanza  majaribio ya chanjo yake ya kutibu na kukinga ugonjwa wa covid-19.

Majaribio hayo yataongozwa na Taasisi ya Utafiti wa Tiba (KEMRI) na kuwashirikisha wataalamu na wahudumu wa afya zaidi ya 400 waliopo kwenye kaunti za Mombasa na Kilifi.

Maeneo ya Pwani nchini Kenya ndiyo yaliyokuwa ya mwanzo kuripoti maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19.

Bodi ya Dawa na Sumu Kenya ilichapisha kwenye mtandao wake mwanzoni mwa wiki hii kuwa, serikali imetoa ridhaa ya kufanyika majaribio ya chanjo hiyo.

Kwenye taarifa yake, Katibu Mwandamizi katika Wizara ya Afya, Rashid Aman, alithibitisha taarifa hizo.

Juni, mwaka huu, Afrika Kusini ilianza majaribio ya chanjo hiyo katika Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza.

Kampuni ya dawa ya AstraZeneca iliyoshirikiana na Chuo Kikuu cha Oxford kuiandaa chanjo hiyo, ilisema majaribio hayo yalisitishwa kwa muda ili kuipa kamati maalumu muda wa kutathmini usalama wake.

Kwa Kenya, majaribio hayo pia yatatathmini usalama wa chanjo yenyewe, uwezo wa kumlinda mhusika na utendaji wake hasa kwa watu wazima walioambukizwa virusi vya corona.

Watu watakaojitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo hiyo, watapewa dozi moja ya chanjo na kufuatiliwa kwa muda wa miezi 12.

Kenya inasisitiza kuwa majaribio hayo ni muhimu ikizingatia maambukizi ya virusi vya corona yamekuwa yakiitesa nchi hiyo kwa muda mrefu sasa.

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi