loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahera: Marufuku lugha zisizo na staha

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini imewapa onyo wanasiasa ambao wanatoa lugha za vitisho, kashfa na kudhalilishana  na kuwataka watambue kuwa sheria za nchi zipo na zinafanya kazi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo  Dk Wilson Mahera wakati akifungua mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ikiwapiga msasa watoa  huduma  mtandaoni , jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 15.

“Mkiona kuna mgombea tunamshuhulikia msishangae, tutaanza kuchukua hatua kali ikiwemo kusitisha mikutano yao ya kampeni,” amesema

Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa kutumia lugha zisizotakiwa kwenye kampeni kinyume na maadili hali ambayo hawatovumilia kuona ikiendelea.

“Wanasiasa wanapaswa kutumia kipindi hiki kunadi sera na ilani zao kwa wananchi ili waweze kuwachagua na si kutukana, kuchochea vurugu au kukejeli wagombea wengine.

“Kuanzia sasa hivi, tutachukua hatua kali kwa wanaotoa lugha kali ikiwemo kumfungia kupiga kampeni na hata ukipiga kelele kwa mjomba huko nje hatutakusikia. Kwa hiyo, wanasiasa wanapaswa kutumia lugha zenye staha,” amesisitiza Dk. Mahera

Aidha Dk Mahera amewataka wagombea ubunge na udiwani waliokata rufaa kuwa na subira  wakati rufaa zao zinashugulikiwa.

“Uchaguzi ni mchakato unaohusisha mambo mengi ikiwemo uteuzi wa wagombea, uandikishaji wapiga kura na kampeni za uchaguzi,” amesema Dk Mahera

Amesema, baada ya uteuzi wa wagombea, walipokea rufaa zaidi ya 500 za wagombea ubunge na udiwani ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi na wanatarajia kuzimaliza kesho Jumatano.

“Wanapokuwa wanatoa matamko yao kuwa tunachelewa kutoa uamuzi wa rufaa watambue tunazifanyia kazi kwa kuzichambua kwa kina ili tuweze kutenda haki.

“Tungepokea rufaa na kukubaliana nazo tungekuwa tumemaliza kuzitolea uamuzi, kwa hiyo watambue tunaendelea kuzifanyia kazi kwa umakini mkubwa na kesho tutamaliza,” amesisitiza

Kauli ya Dk. Mahera imekuja  ikiwa ni siku moja imepita tangu John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema kuitaka Tume hiyo kutoa rufaa hizo haraka ili wahusika waanze kampeni.

Jana Jumatatu, Mnyika alisema, rufaa zao wameziwasilisha NEC lakini hakuna majibu yanayotoka jambo linaloweza kusababisha uvunjifu wa amani.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi