loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Muleba msirudie Makosa

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, John Magufuli amewataka wananchi wa Muleba kutorudia makosa na kuchagua mgombea wa upinzani.

 “Nafahamu tulikuja tukawaomba kura na mimi nilipita hapa nikamuomeba kura mgombea ubunge bahati nzuri mlipa wa CCM, nikaomba mumpe diwani wa CCM bahati mbaya mambo hayakwenda hivyo mkasema hapana,” amesema Magufuli na kuongeza

“Lakini kwa sababu nchi hii ya demokrasia na sisi ni wavumilivu tukasema mtoto akikosea haumkati mkono mtu akifanya makosa husamehewa;…”Ndio maana alimua kutoa Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kujenga Hospitali gombea,”

“Nilipoletewa bajeti kwenye kata hii inataka hospitali nilitoa Shilingi Milioni  500 nikajenga hospitali, nasikia aliyekuwa diwani hapa alisema alileta yeye,”.

Aidha, Mgombea huyo wa Urais kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema aliamua kujenga hospitali hiyo kwa sababu aliona wananchi wanateseka ihali walimchagua kuwa rais na Mbunge wa Muleba Kusini, Anna Tibaijuka, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Kosea njia, kosea kuoa au kuolewa unaweza kutoa talaka au kukataa mume lakini usikosee kuchagua, saa nyingine mnanipa shida kusaidia jimbo unakuta diwani ukisema CCM oye anakunyooshea vidole viwili, amesema Magufuli.

Kufuatia hali hiyo mgombea huyo wa Urais wa CCM amewaomba wananchi wa Kasharunga kuwachagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments