loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kagere aanza kuwindwa

WAKALA wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amesema zipo timu zinataka kuingia mkataba wa awali na mchezaji huyo ila amekataa kwa kuheshimu waajiri wake Wekundu wa Msimbazi.

Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Simba ila kumekuwa na madai ya sintofahamu ndani ya kikosi hicho kwa madai kuwa haelewani na kocha wake, Sven Vandebroeck, ambaye licha ya kuwa mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo amekuwa akimuweka benchi.

Akimzungumzia mchezaji wake huyo, Gakumba alisema mkataba utaisha mwakani na kwamba hataki mambo ya kusaini mkataba wa awali kama ambavyo baadhi ya timu zinataka.

“Simba ni timu nzuri tunaiheshimu, wanakidhi mahitaji ya mchezaji kama tulivyokubaliana, mambo ya kutoenda uwanjani sio yao bali ni ya kocha,” alisema.

Akijibu tuhuma za kutompanga Kagere, Vandebroeck alisema anachoangalia sio mchezaji mmoja, bali timu, huku akisema anapanga kulingana na ubora unaooneshwa na mchezaji.

Kagere amekuwa haanzi kikosi cha kwanza tangu kuwasili kwa kocha huyo katikati ya msimu uliopita na hata katika mechi mbili za msimu huu.

Inadaiwa nyota huyo wa Rwanda anawekwa nje na mfumo wa kocha anayetumia mshambuliaji mmoja mbele na nafasi hiyo akipewa nahodha John Bocco.

Hata hivyo malalamiko yamekuwa mengi miongoni mwa mashabiki na wanachama wa Simba, wakimtaka kocha huyo kumtumia Kagere wakiamini ni mfungaji mzuri kuliko Bocco.

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar imesema mchezo ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi