loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Diamond aingia anga za Aliciakeys

ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla ya msanii wa Marekani, Alicia Keys, kuachia albam ya ‘Alicia’, nyota wa Tanzania, Nassibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’, naye yumo ndani ya albam hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wasafi Tv kupitia mtandao wao wa kijamii wa Instagram, Diamond, ni miongoni mwa wasanii walioshirikishwa katika albam hiyo, akiweka rekodi ya kipekee ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushirikishwa na msanii huyo mkali duniani.

Moja ya nyimbo aliyoshirikishwa Diamond na mshindi huyo mara 15 wa tuzo za Grammy inaitwa ‘Wasted energy.’ Diamond pia ni msanii pekee wa Afrika aliyeshirikishwa kwenye album hiyo inayotarajiwa kuwa na nyimbo 15, huku ikiwa imeshirikisha wanamuziki saba pekee.

Album ya ‘Alicia’ itakuwa ya 13 kwa msanii huyo wa Marekani. Albam yake ya mwisho aliitoa mwaka 2017 ilikuwa ikiitwa ‘Dirty Dancing 2’.

Diamond amewahi kufanya kazi na wasanii wengine wakubwa, hivyo nyota yake inazidi kung’ara kwa kushirikishwa na nguli huyo.

Baadhi ya wasani wakubwa wa bara la Amerika aliowahi kufanya nao kazi ni Omario na Neyo katika wimbo wa African beauty na Marry you zinazofanya vizuri mpaka sasa.

Hao ni baadhi tu, laikini wapo wengi amekuwa akishirikiana nao na yote hiyo ni kutaka kutangaza muziki wake na wa Tanzania duniani kadiri miaka inavyosogea.

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar imesema mchezo ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi