loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mradi kuhamasisha ujasiriamali waja

MJASIRIAMALI maarufu nchini, Maida Waziri amebuni mpango wa kuwafanya vijana kufuatilia ndoto za ujasiriamali kupitia mradi wa Akili ya Pesa Challenge.

Mradi huo utahusisha uwasilishaji wa mawazo ya ujasiriamali kwa vijana kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 na utatumia nguvu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kushirikisha mawazo kiushindani.

“Lengo la mradi ni kuhamasisha ujasiriamali Afrika Mashariki, lakini tunaanzia nyumbani. Tunaamini vijana wana ndoto za kuwa wajasiriamali wakubwa, lakini hawana uhakika, tunataka kuwapa uhakika huo ili wachakarike na kuongeza fursa za ajira,” alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mradi huo ambao uko katika mfumo wa Shindano umeanza jana na unatarajia kumalizika Oktoba 15, mwaka huu na mshindi kuondoka kibindoni na Sh 100,000.

Katika mradi huo vijana watakuwa wanaandika mawazo yao ya ujasiriamali namna ya kutumia fursa kukabiliana na mahitaji ya sasa na ya baadaye katika jamii na mwenye wazo zuri zaidi, atakuwa mshindi.

Kwa mujibu wa Maida, ili kuwezesha vijana kuwa wajasiriamali ni vyema kubadilisha mitizamo yao juu ya namna ya kuanza na kufuatilia ndoto zao, na Akili ya Pesa Challenge ni mwarobaini wake.

“Takwimu za NBS zinaonesha asilimia 60 ya watu nchini ni vijana kati ya miaka 15 hadi 35, hivyo tutatumia nguvu ya Akili ya Pesa Challenge kupanda mbegu ya ujasiriamali ili kuboresha maisha ya vijana, familia na taifa kwa jumla,” alisema.

“Maneno yangu kwa vijana siku zote ni uanze kidogo na kisha ukue. Haijalishi umeanza na kiasi gani cha mtaji, lakini la maana ni kujitambua na kutambua uelekeo wako hivyo kuwa tayari kutekeleza ndoto yako,” alisisitiza Maida.

Kwa mujibu wa Maida, suluhisho la ukosefu wa ajira Afrika (Tanzania ikiwamo) ni kuamsha moyo wa ujasiriamali miongoni mwa vijana.

Akili ya Pesa Challenges imelenga kuweka wazi ndoto za vijana, wajitambue na kuzitumia fursa ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi