loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hotuba ya Dk Mwinyi yawapa matumaini vijana

MKUTANO wa ufunguzi wa kampeni za mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi (pichani), umeleta matumaini kwa vijana visiwani hapa.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mussa Haji Mussa, alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu hotuba ya ufunguzi wa kampeni za mgombea huyo, uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti.

Alisema katika hotuba yake, Dk Mwinyi aliahidi kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa vijana katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ujasiriamali, viwandani, utalii, mafuta, uvuvi na mengineyo.

“Vijana wengi wamefurahishwa na kupata matumaini makubwa juu ya mikakati ya mgombea urais wa CCM katika kuzalisha ajira zaidi ya 300,000 zikiwemo katika uvuvi wa Bahari Kuu.”

“Ni kweli eneo la uvuvi wa Bahari Kuu halijafanyiwa kazi vya kutosha ikiwamo sekta ya uvuvi na uwekezaji, tukifanikiwa katika eneo hilo pamoja na ujenzi wa bandari za uvuvi tutaweza kuongeza ajira,’’ alisema.

Alisema, juhudi za kuwawezesha vijana zimechukuliwa na awamu zote za viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliopita, ikiwamo fedha za Mfuko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kuwezesha wananchi.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kusini, Ibrahim Juma, alisema ajira kwa vijana ni changamoto inayohitaji kufanyiwa kazi ili kujenga ustawi wa kundi hilo.

“Kwa mikakati ya mgombea wetu wa urais Dk Mwinyi, fursa nyingi za ajira zitatengenezwa kwa vijana, hivyo wananchi tumpe kura nyingi apate ushindi wa kishindo ili aweze kuleta neema kwa Wazanzibari,” alisema.

Katibu Mwenezi wa UVCCM wilaya ya Kati Unguja, Haji Abdallah Iddi, alisema vijana wengi wapo mitaani, hivyo wamepata matumaini mapya kuwa Dk Mwinyi akiwa Rais atatafuta ufumbuzi wa tatizo la ajira.

‘’Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, matarajio yake makubwa ni kuona tatizo la ajira linapatiwa ufumbuzi moja kwa moja,’’ alisema.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika uwanja wa Demokrasia wiki iliyopita, Dk Mwinyi alisema anakusudia kutengeneza ajira 300,000 kwa vijana visiwani humo.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi