loader
Amani ilindwe kwa gharama yoyote

Amani ilindwe kwa gharama yoyote

S IKU zote Tanzania imekuwa ikisifi ka kuwa nchi ya amani na imekuwa mhimili mkubwa kwa kueneza amani kwa nchi nyingine katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla. Zipo alama mbalimbali ambazo Tanzania imeacha kwa nchi nyingine, kwa kuhimiza wananchi wa nchi hizo kusimamia amani, wengine wakisuluhishwa kwa namna moja au nyingine, jambo ambalo limekuwa na manufaa makubwa na kuiacha nchi kuwa kitovu cha amani. Aidha, zipo nchi za Afrika ambazo zinaitazama Tanzania kwa jicho la peke yake, kutokana na kuweza kusimamia na kulinda amani iliyopo, lakini pia wakiitazama kwa kujifunza, jambo ambalo limenufaisha wengi.

Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, amani ni jambo muhimu la kuzingatiwa kwa kuwa ni lenye manufaa na kila mmoja anatakiwa kulisimamia kwa nguvu, kuhakikisha amani iliyopo haitetereki na taifa litaendelea kuwa na historia ya kuwa lenye amani wakati wote.

Kama ambavyo Tanzania imeweza kusimama kidete kuhakikisha baadhi ya nchi za Afrika zinakuwa na amani, vivyo hivyo kuelekea uchaguzi huu kila mmoja anatakiwa kutambua wajibu wake wa kulinda amani iliyopo na kuwabeza wenye nia ovu wanaotaka kuyumbisha amani.

Haitarajiwi katika kipindi hiki ambacho kampeni zinaendelea kwa vyama mbalimbali, kuwepo na lugha mbaya zenye kusababisha kutoelewana baina ya makundi.

Badala yake kampeni zinatakiwa kuwa za kistaarabu na zenye kuelimishana kuhusu ilani za vyama husika. Haitarajiwi kupitia kipindi hiki, kuibuke kikundi cha watu kitakachokuwa chanzo cha kuvuruga amani lakini wote kwa pamoja kushikamana kwa kuhakikisha amani inakuwepo na masuala mengine yanaendelea.

Aidha, katika kuhakikisha amani ni jambo muhimu, viongozi wa dini wanashiriki kuwaelimisha waumini wao kuhusu umuhimu wa amani na kutokubali kwa namna moja kuacha nchi kuingia katika mifarakano, kwa kuwa madhara yake ni makubwa zaidi.

Ni wazi kuwa katika kampeni, vipo vyama mbalimbali vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi na kila chama kina ilani yake na maono yake wakati huu wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Kwa misingi hiyo, si jambo la busara kwa wagombea kutumia wasaa wanaoupata wa kampeni kwa kutoa lugha za kejeli, za matusi au zenye kusababisha chuki kwa namna moja au nyingine.

Bali, kinachotarajiwa ni kwa kila mmoja kuona amani ni suala la kipaumbele kwa kila mmoja. Hakuna asiyejua madhara ya nchi kukosa amani, ikiwemo uharibifu wa hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa.

Lakini, pia kuirejesha amani hiyo ni jambo gumu tena linalosababisha athari kubwa. Kwa mikutano yake ya kampeni, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amekuwa mstari wa mbele kusisitiza amani kwa kila mmoja na kwamba chama hicho hakitakubali kuona amani inapotea.

Maneno hayo yanatakiwa kuwepo kwa kila mgombea, kwa maana kuwa kila anaposimama kuanza kunadi sera zake, ahakikishe amani iliyopo ni ya muhimu zaidi na isipotee, bali ilindwe hata baada ya uchaguzi.

Si mara ya kwanza kwa Tanzania kuingia katika uchaguzi mkuu, hivyo ni vyema kwa kila kipindi ambacho taifa linasimama kutekeleza azma hiyo ya kidemokrasia, kuona umuhimu wa kuikumbatia amani iliyopo na pia kutambua kuwa yapo maisha baada ya uchaguzi kukamilika

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5225ba2815a696acb0331616b82c620b.jpg

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi