loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mavunde awahakikishia mikopo wakulima wa nyanya

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema iwapo atachaguliwa kuongoza tena jimbo hilo  atahakikisha wakulima wa nyanya  wanapata mikopo ya uhakika ili kuongeza tija ya uzalishaji na uchakataji wa nyanya.

Mavunde aliyasema hayo janakatika  Kata ya Mpunguzi Kampeni za kuwania Ubunge wa Jimbo hilo.

Mbali na nyanya pia ameahidi kukuza zao la zabibu kwa kutafuta masoko ya uhakika na kuwawezesha wakina mama na Vijana kuchakata zabibu na kuuza mchuzi wa zabibu.

Kuhusu miundo mbinu, Mgombea huyo ambae pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira  alisema  atahakikisha anaboresha na  kukamilisha ujenzi wa shule ya Sekondari Mpya ya Nkulabi iliyoanza kujengwa na Mbunge na Wananchi.

"Kuanza ujenzi wa shule ya Msingi Mpya eneo la Mlangwa ili kupunguza mwendo wa wanafunzi kutembea umbali mrefu," alisema Mavunde

Aidha amesema atakamilisha miundombinu ya miradi ya maji katika maeneo ya Mpunguzi B na Nkulabi.

"Nitasimamia  usambazaji wa nishati ya umeme katika maeneo yaliyosalia machache,"alisema

Kuhusu michezo na sanaa amesema  michezo na sanaa kwa kufadhili mashindano mbalimbali kwa lengo la kuikuza.

TIMU ya  Simba imethibitisha kiungo  wake Mbrazili Gerson Fraga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi