loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Singida sasa ni muhimili wa kiuchumi Tanzania

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imeonesha dhamira ya dhati kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea.

Imehakikisha pia dhamira hiyo ya kujenga uchumi imara usio tegemezi, inaenea kwa viongozi wengine, watendaji na wananchi kwa jumla.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na dhamira hiyo, ni kuendelea kukua na kuimarika kwa uchumi unaochochewa na jitihada za Serikali za kuwekeza kwenye miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege sanjari na kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme.

Aidha, kuimarika kwa Shirika la Ndege Tanzania ni sehemu ya mafanikio hayo, kwani Serikali imefanikisha ununuzi wa ndege zinazosaidia kuitangaza nchi, kuongeza mapato ya Serikali, fursa za ajira kwa vijana na kuwa kichocheo kwa sekta nyingine zikiwamo kilimo, utalii, mifugo na uvuvi.

Katika hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema katika Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kutekeleza Mradi wa Umeme wa Maji wa Mto Rufiji, ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa (SGR), barabara na kukuza sekta ya anga.

Waziri Mkuu anasema: “Utekelezaji wa miradi hiyo ya miundombinu wezeshi ya kiuchumi unalenga kufungamanisha ukuaji wa sekta hizo na sekta nyingine hususan za biashara, kilimo na utalii.

Aidha, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro na Morogoro-Makutupora ya Singida unaendelea vizuri na kwa kasi ya kuridhisha.”

Mara kadhaa Majaliwa amekuwa akisisitiza kuwa, kuimarika kwa sekta hizo kutachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa jumla.

Amekuwa akitoa rai kwa wabunge, wafanyabiashara na wajasiriamali, viongozi na watendaji wa serikali, taasisi za dini, asasi za kiraia, washirika wa maendeleo, na wananchi wote kwa jumla, kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza mpango huu ili kufikia uchumi wa juu unaoongozwa na viwanda baada ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi anasema katika kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu anatembelea katika mikoa ya kati hususan Mkoa wa Singida katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya Itigi, Itaja, Ilongero na Mkalama, ni dhahiri atashuhudia mageuzi makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Anasema Singida ya sasa ni tofauti na Singida ya awali kwani imebadili taswira yake na kuwa muhimili wa uchumi wa Tanzania.

“Niseme tu kwamba, Singida ya sasa ni njema na ni njema sana kwani siyo kwamba ni katikati ya nchi yetu, bali kutokana na mapinduzi ya kiuchumi yanayofanyika sasa, Singida inakuwa kitovu cha uchumi wa nchi yetu kinachounganisha nchi zote za Afrika kwa jumla,” anasema.

MIUNDOMBINU NA USAFIRISHAJI

Katika Mkoa wa Singida hali ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji ndani na nje ya Mkoa imeendelea kuboreshwa na kuimarishwa ambapo kwa Barabara Kuu:

Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Singida unahudumia mtandao wa kilometa 1,727.6. Jumla ya km. 7,136.4 zimetengezwa kwa Sh 54,879,601,000 na matengenezo ya madaraja ya aina mbalimbali 238.2 kwa gharama ya Sh 14,863,844,000

Aidha, ujenzi wa Daraja la Sibiti (Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama) umefanyika kwa Sh 28,511,511,000, ujenzi wa Daraja la Msingi (Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama) umefanyika kwa 9,002,573,250, ujenzi wa barabara ya kuingia Hospitali ya Wilaya – Kiomboi (Halmashauri ya Wilaya ya Iramba) Km. 1.7 umefanyika kwa Sh 1,531,498,600, ujenzi wa kituo cha ukaguzi (OSIS) wa Malori Kata ya Muhalala Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Sh 24,431,922,669.76.

Kwa upande wa Barabara za Mijini na Vijijini: Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), anahudumia mtandao wenye jumla ya kilometa 5,599.

Katika utekelezaji wa malengo ya ilani, Sh 15,661,030,000 zimetumika kufanya matengenezo na maboresho ya barabara ambapo matengenezo ya kawaida (kuwekewa changarawe na udongo) kwa km. 1,520 za barabara yamefanyika kwa Sh 4,847,940,000.00. Matengenezo ya sehemu korofi na matengenezo maalumu km. 417.8 yamefanyika kwa Sh 4,888,530,000.00. Madaraja mawili yametengenezwa, makalvati 52 na vivuko 6 vimetengenezwa kwa Sh 3,666,560,000.00.

Ujenzi wa barabara za lami katika Miji ya Mkalama na Itigi Km. 2.1 (Itigi Km. 1.1 na Mkalama Km 1.0) umeanza kwa Sh 1,000,000,000.00.

Aidha, katika Manispaa ya Singida, barabara zenye urefu wa km. 9.1 zimewekewa taa za barabarani 253 kwa Sh 1,258,000,000.00.

NISHATI (UMEME)

Kuhusu nishati (umeme) Dk Nchimbi anasema katika kipindi cha miaka mitano (2015-2020), umefanyika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kusambaza umeme, kuboresha nguvu ya umeme, kukarabati miundombinu na kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme wa uhakika na kupelekea kutokuwa na tatizo la ukatikaji wa umeme unaotokana na upungufu katika uzalishaji wa nishati ya umeme.

“Pamoja na miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini, Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miaka mitano imetekeleza miradi ya usambaji wa umeme katika Mkoa wa Singida,” anasema Dkt Nchimbi.

Anaainisha kuwa, Sh 39,326,618,982 zimetumika kutekeleza Miradi ya REA II, Sh. 41,834,641,177 zimetumika kutekeleza Miradi ya REA III. Jumla ya Sh. 12,924,115,793 zimetumika kutekeleza Miradi ya “Backbone.”

Anafafanua kuwa, kupitia miradi hiyo maeneo mbalimbali yamenufaika katika Mkoa wa Singida yakijumuisha Hospital za Wilaya 2 zilizofikiwa na huduma ya umeme (Hospitali ya Wilaya ya Singida – Ilongero na Hospitali ya Wilaya ya Mkalama), shule za msingi na sekondari 52 zimefikiwa na huduma ya umeme, vyanzo vya Maji 11 (Manispaa ya Singida 2- )

“MZAZI anadhani ni bora ampe mtoto ...

foto
Mwandishi: John Mapepele, Singida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi