loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watu 5 wafa ajalini Mtwara

WATU watano wamepoteza maisha baada ya mabasi wawili kugongana katika Kijiji cha Msanga kata ya Mitesa wilayani Masasi, Mtwara.

Ajali hiyo ilitokea Septemba 15 mwaka huu saa 7:00 mchana kwenye barabara ya Newala-Masasi, watu watano wakafa papo hapo na wengine sita walijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Mark Njera (ACP) amesema ofisini kwake kuwa gari mojawapo lililohusika kwenye ajali hiyo ni aina TATA lenye namba za usajili T 714 DEH lililokuwa likiendeshwa na Hamisi Salum (31).

Gari hilo linafanya safari zake kutoka Masasi kwenda Newala. Liligongana na basi dogo aina ya Isuzu Jorney AER lenye namba za usajili T 311 AER lililokuwa likitoka Newala kwenda Kijiji cha Mchahuru wilayani Masasi.

Kamanda Njera alisema hali za majeruhi majeruhi watano walifikishwa katika hospitali ya Newala kwa matibabu na wanne hali zao zinaendelea
vizuri.

“Kwa mujibu wa taarifa ya asubuhi ya leo (jana) majeruhi watano waliofikishwa kwenye hospitali ya Newala majeruhi wanne hali zao zinaendelea vizuri
kwa hiyo huenda leo wakaruhusiwa na mmoja ataendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo”alisema na kuongeza;

“Na huyo majeruhi mmoja aliyoko Mkomahindo nimepata taarifa kuwa kuna mpango wa kumpeleka hospitali ya Ndanda kwa ajili ya uchunguzi zaidi
lakini wote hali zao siyo mbaya wanaendelea vizuri”

Alisema, chanzo cha ajali hiyo ni kwamba gari hilo aina ya TATA lilipoteza mwelekeo na kugonga gari lingine Isuzu Jorney ubavuni.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Mtwara

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi