loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KQ yaruhusiwa kutua tena nchini

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inasubiri maombi na ratiba kutoka Shirika la Ndege la Kenya (KQ) ili kufahamu idadi ya safari za shirika hilo, baada ya kuruhusiwa kuanza tena kutua nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo kuruhusu kuanza tena kwa safari za Kenya Airways nchini

Johari alisema kutokana na hali ya kibiashara, ikizingatiwa athari za virusi vya corona kwa usafiri wa anga, KQ italazimika kupeleka ratiba ya ndege zake zitakazoingia nchini kwa siku au kwa wiki.

“KQ watalazimika kuleta maombi yanayoonesha ratiba yao jinsi watakavyofanya kazi hapa nchini, kipindi kile (Agosti Mosi) walileta maombi yanayoonesha ratiba yao kuwa watafanya safari kuja Tanzania mara saba kwa siku, ikiwa ni mara tatu Dar es Salaam, mara mbili mkoani Kilimanjaro na mara mbili Zanzibar,” alisema.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema ingawa serikali ya Kenya imeondoa sharti la kukaa karantini kwa siku 14 kwa abiria kutoka Tanzania, ratiba yao kwenda Kenya itaanza Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema safari za ATCL kwenda Kenya zinazingatia mpango wa kibiashara, ambao tangu awali ulionesha kuwa safari hizo zitaanza mwezi huo.

“Mipango yetu kwa Kenya inakwenda kutokana na mpango wa kibiashara kwa hiyo haina mabadiliko. Tulitegemea kuanza safari zetu mwezi wa 12, kwa hiyo hilo lipo palepale, tunasubiri muda ufike tutoe taarifa,” alisema Matindi.

Awali TCAA ilitoa taarifa ya kutengua amri ya kuzuia ndege za Kenya kutua nchini, kutokana na tangazo kama hilo lililotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya, kuondoa kigezo cha kuwekwa karantini kwa abiria wote kutoka Tanzania watakaowasili huko.

Kutokana na tangazo hilo, kampuni za KQ , Fly 540 Limited, Safarilink Aviation na AirKenya Express Limited, zimeruhusiwa kufanya safari zake Tanzania.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro, Tudarco

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi