loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM akistaafu kuishi Kagera

RAIS John Magufuli ameweka wazi kwamba akistaafu utumishi wake wa urais, atakwenda kuishi mkoani Kagera, kwa kuwa anapapenda na ameweka vitega uchumi vyake ikiwemo mifugo.

Aidha, alisema yapo maneno kwamba fedha za misaada, zilizotolewa na wahisani mbalimbali kwa ajili ya athari za tetemeko la ardhi lililoikumba mkoa huo Septemba mwaka 2016 zimeliwa, sio za kweli, bali zilitumika kutekeleza miradi ya msingi mkoani humo ikiwemo ujenzi wa shule.

Aliyasema hayo jana mjini Bukoba mkoani Kagera, alipoomba kura kwa maelfu ya wananchi waliofika Uwanja wa Gymkhana kusikiliza sera za mgombea huyo wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Magufuli alisema, “nimekuja hapa kwa ukumbusho mkubwa, hapa ndipo mahali  nilipewa warranty (hati) ya kusafiria kwenda kusoma Mkwawa High School…nimepanga baada ya kustaafu nitakaa Kagera na ndio maana nina ng’ombe wangu huku, ninapapenda, na watu wa Kagera ni wazuri wanahitaji maendeleo  na uchumi,” alisema Rais Magufuli aliyewahi kuwa Mbunge wa Biharamulo Mashariki mkoani Kagera.

Alisema mkoa huo anaupenda, ndio maana hata alipokuwa akitafuta Katibu Mkuu wa CCM, aliangalia maeneo mengi ya nchi na akamuona Dk Bashiru Ally ataweza, ndio maana alimchagua; na anatoka Kagera.

“Ninapapenda Kagera, hata nilipokuwa natafuta Katibu wa chama niliangalia wee nchi nzima, nikamuona Dk Bashiru ataweza, ametoka maisha ya chini, amefanya biashara ya ndizi pale Kemondo, ni mzalendo kati ya wachache wa kufuata miiko ya Mwalimu Julius Nyerere, ndio maana nikamteua awe Katibu Mkuu wa CCM,” alisema Rais Magufuli akimuelezea mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aliwaomba kura ya ndio wananchi, akiahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu iwapo watamchagua. Alisisitiza kuwa hataongeza hata siku moja baada ya kipindi hicho  kumalizika

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi