loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

PBZ kufikia mikoa nane Bara

BENKI ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) imeanza kutoa huduma za kibenki kupitia Shirika la Posta Tanzania katika mikoa minane ya Tanzania Bara.

Hatua hiyo inatokana na benki ya PBZ kuingia mkataba na Shirika la Posta Tanzania na kuzindua uwakala wa huduma za kibenki katika shirika hilo juzi.

Akizungumza baada ya kuzindua huduma hiyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Mwinyi Talib Haji, aliitaka PBZ kutafuta sehemu mtambuka za uwekezaji ili kuwawezesha wananchi kupata huduma.

Alisema wananchi wamekuwa wakichelewa kupata huduma kutokana na kuchelewa kuanzishwa ushirikiano huo, hivyo waangalie sehemu nyingine zenye fursa ili kuwekeza kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.

"Hatuwezi kuendelea kuchelewa kuwapatia wananchi huduma kwa sababu hatuna tawi, hivyo kwa njia hii tunaweza kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo ambayo ni mtambuka kwa faida ya serikali zetu yaani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania… Ni wakati sahihi kuangalia na maeneo mengine," alisema Dk Haji.

Akaongeza: "Tunataka mteja akiingia kwenye taasisi moja, anapata huduma zote anazozitaka, jambo hili litamrahisishia mwananchi huyu kutunza muda na kufanya shughuli nyingine za maendeleo."

Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang'ombe, alisema ushirikiano huo ni mwanzo mzuri wa kifikisha huduma kwa urahisi kwa wananchi.

 Mwang’ombe alihidi Shirika la Posta kutoa huduma za kibenki za PBZ bora huku akitoa rai kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano na taasisi zao, kulitumia shirika hilo kusafirisha barua, vifurushi na vipeto.

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Iddi Haji Makame alisema: "Kwa ushirikiano huu, tunaamini huduma za kibenki za PBZ zitakuwa kwa kasi Tanzania Bara, Benki yetu iko katika ATM ya Umoja Switch ambazo ziko 260, lakini kwa kuongeza ofisi za Shirika la Posta, huduma zetu zitazidi kuimarika kuliko kutumia wakala mmoja mmoja."

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PBZ, Kidawa Hamidi Saleh, kwa kaunzia huduma hizo za uwakala zitapatikana katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Tanga, Lindi, Arusha, Morogoro na Mtwara.

"Kujenga tawi moja inagharimu takriban Sh bilioni 3, lakini kupitia ushirikiano huu itakuwa rahisi kwetu kuwafikia wananchi tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Saleh.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia sekta ya mawasiliano, Dk Jimy Yonazi alipogeza ubunifu kwa kuongeza huduma kwa kushirikiana na taasisi za fedha.

 

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Anastazia, Anyimike, Dodoma

2 Comments

 • avatar
  hghgh
  18/09/2020

  comment is too short

 • avatar
  hghgh
  18/09/2020

  comment is too short

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi