loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NBC yawapa mafunzo wachimbaji Geita

WAJASIRIAMALI na wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita, wameanza mafunzo maalumu yanayolenga kwa kuwajengea uwezo wa  kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa viwango shindani vya kimataifa.

Mafunzo hayo ya siku tatu, yameandaliwa na Benki ya NBC na wadau wengine. Yalizinduliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel kwenye Maonesho ya Dhahabu na Teknolojia, yanayofanyika mkoani humo.

Gabriel alitoa wito kwa wafanyabiashara na wachimbaji wadogo mkoani humo, kuzingatia kanuni za utunzaji wa fedha na heshima ya matumizi ili kulinda na kukuza mitaji yao.

“Ninaomba sana wajasiriamali na wachimbaji wadogo kupitia mafunzo haya mbadilike na mtoke kwenye mfumo wa kufanya shughuli zenu kwa mazoea na badala yake mhamie kwenye mfumo wa kisasa unaoheshimu ushauri wa wataalamu wakiwemo hawa wanaotoka kwenye taasisi za fedha kama benki ya NBC na taasisi na mamlaka nyingine zinazosimamia biashara nchini,” alisisitiza.

Alisema iwapo wadau hao watatumia vizuri rasilimali madini hususani dhahabu, ni rahisi kwao kufanikiwa na kutoa mfano wa mabadiliko ya kisera na kiutendaji, yalivyoongeza mapato yanayopatikana kutokana na madini katika mkoa huo.

Alitaja baadhi ya mada muhimu kwenye mafunzo hayo kuwa ni taratibu bora za uchimbaji madini, umuhimu wa ulipaji kodi na taratibu za kufuata, matumizi sahihi ya taasisi za kifedha na upatikanaji wa mitaji, umuhimu wa kuwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na matumizi sahihi ya kemikali katika shughuli za uchimbaji madini.

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje alisema katika mafunzo hayo watatambulisha fursa za huduma na bidhaa za kibenki ikiwemo huduma ya Klabu ya Biashara, ‘internet banking’ na mikopo isiyo na dhamana kutoka benki hiyo.

Pia, alisema mafunzo hayo yatawasaidia walengwa hao kuzitambulisha fursa za kibiashara ambazo wajasiriamali na wachimbaji wadogo hususani wa mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wanaweza kunufaika nazo.

Mbali na NBC,  mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu mbalimali kutoka TANTRADE, Tume ya Madini, TRA, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, GST, SIDO, NEMC, TBS, OSHA, NEEC na taasisi nyingine za kifedha.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi