loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Thiago, Liverpool kimeeleweka

LIVERPOOL inakaribia kumsajili kiungo wa Hispania, Thiago Alcantara, kutoka Bayern Munich, kwa ada ya pauni milioni 27.

Thiago, 29, alijiunga na miamba hiyo ya Ujerumani akitokea Barcelona mwaka 2013 na kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, ambapo Bayern iliibuka na ushindi dhidi ya Paris St-Germain.

Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Liverpool na Bayern juu ya mchezaji huyo, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Thiago atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu England, baada ya beki wa kushoto wa Ugiriki, Kostas Tsimikas.

Alipoulizwa kuhusu umahiri wa Thiago wiki iliyopita, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alisema: "Siwezi kuzuia tetesi hasa kipindi hiki cha dirisha la usajili, ni wazi nimewahi kusema mahali kwamba Thiago Alcantara ni mchezaji mzuri zamani sana.”

"Ni vizuri kwamba tunahusishwa nae ni kwasababu ni mchezaji mzuri bila shaka na Liverpool ni klabu kubwa, kwa hiyo sio jambo baya.”

Thiago alianza maisha yake ya soka Barcelona na wakati fulani aliwahi kuhusishwa kutaka kuhamia Manchester United wakati David Moyes alipochukua timu kwa Alex Ferguson mwaka 2013, lakini uhamisho huo haukufanikiwa badala yake akaenda Ujerumani.

Mbali na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameshinda mataji mengi mfululizo ya Bundesliga,  manne ya kombe la Ujerumani na Kombe la Dunia ngazi ya klabu akiwa na Bayern.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amejikuta katika wakati mgumu baada ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi