loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam FC yaiwaza Mbeya City

TIMU ya soka ya Azam FC imesema mchezo ujao dhidi ya Mbeya City unaweza kuwa mgumu, ila watalazimisha kupata matokeo mazuri.

Kocha msaidizi wa kikosi hicho, Vivier Bahati, alisema Dar es Salaam jana kuwa, ugumu wa mchezo huo utakuja kutokana na timu hiyo kupoteza michezo miwili ya awali, hivyo itataka kupambana kutafuta pointi tatu.

Mbeya City ilipoteza michezo miwili ya ufunguzi dhidi ya KMC ilipofungwa mabao 4-0 na dhidi ya Yanga bao 1-0 na itakutana na Azam FC katika mchezo wa nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya keshokutwa.

“Mbeya City wametoka kupoteza michezo miwili, tunajua mchezo hautakuwa rahisi ila tutalazimisha iwezekanavyo kupambana na kupata matokeo mazuri,” alisema.

Alisema wanajua pia uwanja wanaokwenda kukutana nao sio mzuri na ndio maana waliamua kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp kwenye uwanja unaofanana na utakaotumika katika mchezo huo.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa juzi, Azam FC ilifungwa mabao 2-1, ikiwa ni sehemu ya mazoezi kabla ya kukutana na Mbeya City.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka leo kwa basi kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo muhimu wa Ligi Kuu kwa ajili ya kupigania kupata pointi tatu.

Azam FC inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania bao 1-0 na dhidi ya Coastal Union 2-0.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 15 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 15 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...