loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea mwenza Chadema awapongeza Polisi

MGOMBEA Mwenza wa urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kuimarisha ulinzi na usalama tangu alipoanza ziara ya kampeni mkoani mkoani hapo.

Aliyasema hayo akiwa katika mkutano wa kampeni wilayani Babati na akasema tangu alipoanza mikutano ya kampeni hakuwahi kupata ushirikiano kama alioupata Manyara.

"Nataka niwahakikishie tangu nimeanza ziara hii sijapata ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi kunilinda mimi mwenyewe, kunilinda nikiwa njiani na kulinda mikutano yangu kama nilivyoingia mkoa wa Manyara kuanzia leo asubuhi, wamenilinda mbele na nyuma wakati wote wa msafara ninawashukuru na  hili ndio Jeshi la Polisi tunalohitaji”alisema na kuongeza;

"Ndio maana Chadema tunataka tuwabadilishieni mfumo wa Jeshi la Polisi tuliondoe kwenye police force liwe ni jeshi la kuhudumia watu ili tulinde masilahi yenu,tuwaondolee msongo wa mawazo na tuwarudishie heshima yenu''alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema Chadema kikichaguliwa wanataka kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala kwa kuwa wanaamimi kuwa ukiwa na kiongozi lazima uamini katika sheria na haki ili watendaji wa chini wafanye hivyo hivyo.

Aliomba wananchi wawachague madiwani wa chama hicho ili wakasimamie fedha za maendeleo.

Mwalimu alisema Chadema ikichaguliwa watumishi wa umma watapata stahiki zao ikiwa ni pamoja na kuongezwa mishahara.

"Mtumishi umehamishwa kituo cha kazi bila kulipwa masurufu yako,tutakulipa fidia ,mtumishi unayepandishwa daraja bila nyongeza ya mshahara miaka mitano tutakulipa fidia kupanga ni kuchagua  sisi tumechagua maendeleo ya watu  na siyo maendeleo ya vitu"alisema

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mariam Juma, Babati

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi