loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea CUF kuhimiza viwanda vya nyuzi, matunda

MGOMBEA ubunge jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Mirambo Yusuph amesema kipaumbele chake kikubwa akichaguliwa ni kurejesha kiwanda cha nyuzi ili wakazi wa manispaa Tabora wapate ajira.

Mgombea huyo ambaye ni mwandishi wa habari za michezo, alisema hayo wakati akizungumza na HabariLEO ofisini kwake eneo la kata ya Gongoni.

Yusuph alisema akiwa Mbunge ataishauri serikali iweke mazingira mazuri ili manispaa ya Tabora iwe na kiwanda bora cha nyuzi kizalishe ajira nyingi kukuza uchumi wa eneo hilo.

Alisema pia ataishauri serikali ipeleke mwekezaji wa kiwanda cha matunda hasa embe kwa kuwa yapo ya kutosha na yamekuwa yakisafirishwa kupelekwa mikoa mingine badala ya kuwa fursa kwa wananchi wa Tabora.

Yusuph pia alisema, ataishauri serikali iweke mazingira mazuri ili wananchi wakopeshwe fedha wafanye shughuli za kuzalisha mali.

Alisema, kwenye uchumi wa Tabora huwezi kuacha kuzungumzia zao la tumbaku hivyo akichaguliwa kuwa Mbunge wa Tabora Mjini atahimiza kufufuliwa kwa zao hilo sanjari na bei nzuri ya zao hilo.

Alitaja kipaumbele chake kingine kuwa ni kuisimamia serikali ili maeneo yote muhimu yenye magari ya wagonjwa yasiyofanya kazi yafufuliwe ili wananchi wapate huduma ya tiba sahihi kwa wakati sahihi.

Yusuph alisema atakapokuwa Mbunge pia atasimamia suala la sheria ya msamaha wa huduma ya afya kwa akina mama wajawazito, walemavu, watoto chini ya miaka mitano, wazee na wahanga wa ajali.

Alitaja kipaumbele chake kingine kuwa ni kuongeza zahanati na vituo vya afya katika kata zote ambazo ziko nje ya manispaa ambazo zinaonekana kama ziko vijijini.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael,Tabora

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi