loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mabula aahidi kujenga barabara, madaraja

MGOMBEA ubunge jimbo la Ilemela, Mwanza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Angelina Mabula amewaahidi wakazi wa kata ya Nyasaka kuwa atajenga miundo mbinu hasa barabara na madaraja.

Mabula alisema hayo wakati wa mkutano wa kampeni katika viwanja vya ukombozi.
Aliahidi atajenga barabara za Mkombozi kwenda Chamwenda na tayari Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) imetenga shilingi milioni 39.4.

Alisema barabara ya Balali mpaka Nyakato imetengewa shilingi milioni 37.6 na itajengwa mwaka huu wa fedha.

Dk Mabula alitaja barabara zingine itakayotengenezwa kuwa ni Nyamuge kwenda Kawekamo.

Dk Mabula alisema wamefanikiwa kuweka lami katika barabara za Big bite-Mji Mwema, Sabasaba- Buswelu, Igombe-Kayenze

Katika sekta ya ardhi Mabula alisema walifanikiwa kuwalipa fidia milioni 65 kwa wakazi 17 waliokuwa na mgogoro wa ardhi katika kata ya shule ya msingi Nyasaka.

Alisema pia mitaa 2,735 imeweza kupewa na wakazi wa maeneo hayo ya mtaa wa Nyasaka na Kiloleli wamepimiwa maeneo yao.

Alisema jumla ya wakazi 59,000 walipimiwa maeneo yao na kupewa hati. Katika sekta ya afya, Dk Mabula alisema wilaya ya Ilemela imefanikiwa kujenga zahanati zaidi ya tano ambazo ni Lukobe, Buganda, Nyamadoke na Lumala.

Aliahidi pia watajenga zahanati moja katika kata ya Nyasaka. Katika elimu alisema wilaya ya Ilemela wamefanikiwa kuongeza shule za kidato cha tano na sita shule mbili ambazo ni Sangabuye na Buswelu.

Alisema katika miaka yake mitano ya uongozi wamejenga vyumba vya madarasa 106.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi