loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ajali za moto mashuleni zitafutiwe mwarobaini

MWANZONI mwa wiki hii taifa lilipatwa na simanzi kubwa kutokana na  tukio la ajali ya  moto, uliotokea katika bweni la Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyopo wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watoto 10 waliokuwemo ndani.

 Huku chanzo chake kikiwa bado hakijajulikana, wakati huu ambapo vyombo vya ulinzi na usalama  vikiendelea kulifanyia uchunguzi, itambulike kuwa tukio hilo la moto shuleni siyo la kwanza kutokea hapa nchini, ikikumbukwa kuwa hivi karibuni moto ulitokea katika shule mbili za Dar es Salaam, ikiwamo ya Ilala Islamic, ambao kama ilivyo kwa shule ya Byamungu, pia ulisababisha vifo.

Mbali na shule hizo, Shule ya Sekondari ya Mivumoni iliyopo Kinondoni, nayo kama ilivyo kwa shule hizo, pia ilipatwa na janga hilo, ingawa halikuwa na madhara  ya kusababisha kifo na hasara ya mamilioni ya fedha, kutokana na kuteketea kwa mali mbalimbali shuleni hapo.

Kwa ujumla, matukio kama hayo yanaweza kuleta hali ya sintofahamu katika jamii kuhusu chanzo chake.

Wakati jamii ikijiuliza kuhusu matukio hayo, rai yangu kwa mamlaka zinazohusika ni kufanya uchunguzi wa kina na kutoa majibu kwa Watanzania ili tuweze kufahamu kuhusu chanzo chake.

 Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kwamba siyo juzi, jana wala leo matukio ya moto kutokea na kuripotiwa hapa nchini, kwani huko nyuma yapo matukio mengi ya ajali hizo zilizowahi kutokea na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari, ambayo kwangu mimi naona yangekuwa somo tosha la kutufanya tuamke na kuwa makini ili yasijitokeze tena mara kwa mara.

Kama tungekuwa tumejifunza kutokana na majanga hayo yaliyowahi kutokea kipindi cha nyuma, haya yanayotokea hivi sasa pengine yasingetokea, kwa kuwa tungejipanga kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana nayo.

Naungana na Rais John Magufuli na Watanzania wote katika kutoa pole kwa ndugu, jamaa na wote waliopatwa na mkasa huo na hata wale waliojeruhiwa Mungu akawaponye upesi waweze kurejea katika afya zao mapema na kuendelea na masomo.

Jambo la msingi hapa ni kwa wakuu na wamiliki wa shule zote zinazingatia agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha mazingira ya shule yanakuwa na vifaa vya kuzimia moto ili pamoja na mambo mengine viweze kusaidia katika uzimaji wa haraka wa moto kabla ya madhara makubwa kutokea.

Ieleweke kuwa tatizo la moto linapotokea hasa nyakati za usiku ni watu wachache wanaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kujitokeza kuudhibiti, hivyo pamoja na uwekaji wa vifaa hivyo, nashauri pia wanafunzi wafundishwe juu ya njia sahihi za kukabiliana na moto pindi unapokea na matumizi ya vifaa hivyo.

Ni imani yangu kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yao kwa umakini mkubwa, nikiamini sababu ya matukio ya moto katika maeneo hayo itajulikana ili kama kuna mtu au kikundi cha watu kimehusika kufanya njama waweze kuchukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi