loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TIC yataja umuhimu wa SGR kukuza uwekezaji

MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dk Maduhu Kazi ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Amesisitiza kuwa uwepo wa mradi huo, utasaidia taifa kupiga hatua kubwa katika suala la uwekezaji.

Dk Kazi alitoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao cha pamoja na wakuu wa taasisi za serikali, kuandaa mpango wa kuibua fursa za uwekezaji zinazotokana na kuwepo wa mradi huo.

Alisema, uwepo wa reli hiyo utaisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo, kwa kuwa ni mojawapo ya maboresho ya mazingira ya uwekezaji.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Kusudi la reli hii ni zaidi ya usafirishaji wa kubeba abiria na mizigo, ndio maana Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimeona ni vema kuibua fursa au shughuli za kiuchumi zinazotakiwa kufanyika katika maeneo ya pembezoni mwa reli ili kuleta ufanisi na tija kwa reli, nchi na jamii iliyopo pembezoni mwa reli hii" alisema Dk Kazi

Alisema SGR ni miongoni mwa maboresho ya mazingira ya uwekezaji kwenye miundombinu, hivyo ni wajibu kila taasisi, wananchi na jamii kujiandaa kuitumia reli hiyo kikamilifu.

Dk Kazi alisema kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji Namba 26 ya mwaka 1997, miongoni mwa majukumu ya TIC ni kuibua, kuhamasisha na kunadi fursa za uwekekezaji nchini. Alisema kikao hicho kililenga kupata mawazo ya pamoja.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, aliipongeza TIC kwa kuratibu mpango huo.

Kadogosa alisema TRC ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha SGR inaleta manufaa zaidi kwa jamii, hasa iliyopo pembezoni mwa mradi huo.

Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede alisema mpango wa utekelezaji wa mradi huo, unapaswa kuishirikisha sekta binafsi na wadau ; na kila taasisi itakayohusika, ipewe jukumu la kutekeleza kwa wakati.

Alisema TRA ipo tayari kushirikiana na TIC, kufanikisha mpango huo wenye nia ya kuifanya SGR isiishie kubeba mizigo na abiria tu, bali iende iwe na faida nyingine za kiuchumi.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi