loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli atamba kutwaa ushindi Uchaguzi Mkuu

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli anaamini atashinda kwa kura nyingi Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Aliyasema hayo jana mjini Kibondo mkoani Kigoma wakati akiomba kura kwa wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa kampeni.

“Kwa sababu urais mimi nitashinda tu”alisema Magufuli na kujivunia namna serikali ilivyotimiza ahadi kwa kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 na ameahidi kutekekeleza ahadi zote za kwenye ilani ya sasa.

Baada ya CCM kumaliza awamu ya kwanza ya kampeni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole alisema kama kura zingepigwa wakati huo Magufuli angeshinda kwa asilimia 85.

Jana jioni wakati akiwa Buhigwe Magufuli alisema, kote alipopita walimweleza watamchagua yeye aendelee kuwa Rais.

“Na mwaka huu ni kama tumeshashinda, na wapinzani wataisoma namba” alisema na kusisitiza wananchi waende kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu.

Magufuli ametaka wananchi wa Kibondo na maeneo mengine ambao bado wanaendelea na makundi ya watia nia waliokuwa wakiomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge kuyavunja na kuwaunga mkono wagombea walioteuliwa kwa kwa kuendeleza makundi kunachelewesha maendeleo.

“Inawezekana hapa kuna makundi bado hayajavunjwa na ndio yanayowachelewesha, masuala ya kugombana ndani kwa ndani kuhusu nani kateuliwa nani kaachwa yanawachelewesha maendeleo, Watanzania wa hapa wote uwe chama chochote, vunjeni makundi muungeni aliyepita, tunahitaji maendeleo,”alisema Magufuli.

Alitoa mfano kuwa hata yeye mwaka 2015 alipotangaza nia walikuwa watia nia 42 lakini akapata yeye, na kwamba, hiyo ni mipango ya Mungu na kutaka wanaCCM  waliokosa wasinune, kwa sababu uongozi ni suala la kupeana kijiti.

Alisema ndani ya miaka mitano miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa wilayani Kibondo ikiwemi ya afya.

Alisema, vituo vitatu vya afya vimejengwa maeneo ya Magenzi , Naruyoba na pia katika Kijiji cha Kigaga na pia upanuzi wa zahanati umefanywa.

Kuhusu, elimu Magufuli alisema shule zimekarabatiwa ikiwemo sekondari ya Malagarasi na Kibondo na pia ujenzi wa hosteli umefanywa eneo la Mkubwa  sanjari  ujenzi wa madarasa.

Magufuli alionesha kukerwa na kasi ndogo ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa wilayani humo. “Pamoja na miradi mingi kutekelezwa hapa Kibondo, lakini sijafurahishwa na kasi ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ndani ya miaka mitano, madarasa tisa tu yamejengwa, ni machache mno,”alisema.

Kuhusu barabara alisema, hivi sasa mradi wa ujenzi wa barabara itakayounganisha Kibondo na maeneo mengine ikiwemo Nyakanazi, inaendelea, na kwamba, katika Ilani ya mwaka 2020-2025 barabara hiyo ipo na zitatumika shilingi bilioni 300.

Alisema umefika wakati wa utajiri kwa wananchi wa Kigoma na amewataka wasiuze mashamba kwa sababu barabara hiyo itakapokamilika itakuwa barabara kuu inayounganisha mikoa, wilaya mfano Bukoba, Biharamulo, Kakonko, Kasulu, Uvinza, Mpanda, Sumbawanga, Tunduma na nchi za Uganda, Sudan, Zambia hadi Afrika Kusini.

“Nawaambia ukweli jipangeni kwa ajili ya kutajirika, limeni, fanyeni biashara ili muuze, mabasi na magari mengine yatapita hapa kwenda mikoa mingine na nchi hizo mtauza, hakuna atakayekuja kuwapa pesa za bure, jipangeni kwa ajili ya kutajirika, tena nyie bahati nzuri ni wachapakazi, mlikosa miundombinu ya barabara ninawaletea na umeme pia,”alisema Rais Magufuli.

Alisema Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na changamoto ya maji na kwamba upo mradi wa kuboresha upatikanaji wa maji ambao umetengewa shilingi milioni 600, na kwamba, mradi huo upo Kibondo.

Kadhalika akizungumzia suala la umeme, Rais Magufuli alisema jumla ya vijiji 43 vimeshapatiwa umeme na vilivyobaki ni saba na kuahidi iwapo atachaguliwa ndani ya miaka michache ya mwanzo vijiji hivyo vote vitakuwa na umeme.

“Ndio maana nasema mnichagulie Mbunge Nditiye(Atashasta), ili iwe rahisi kwangu kumbana na kumwagiza atekeleze changamoto hizo zote zilizobakia, urais au ubunge sio kuangalia sura, changueni maendeleo na mkoa huu mnabahati  mmepata mawaziri watatu,”alisema Rais Magufuli.

Akiwa wilayani Kasulu, Rais Magufuli alisema anatambua kero ya maji iliyopo na kuagiza katika mradi mkubwa wa maji unaojengwa, wananchi wachimbiwe bwawa bure  watakalolitumia kupata huduma hiyo wakati wakisubiri kukamilika kwa mradi husika.

Aliahidi kuwa iwapo wananchi watamchagua kuongoza kwa miaka mitano ijayo, atahakikisha mikakati iliyowekwa ya kufufua uchumi wa mkoa wa Kigoma.

“Msifanye makosa hapa Kasulu, Kigoma ilisahaulika, ni mkoa ulioachwa nyuma kwa miaka mingi, nikasema lazima niweke mikakati mikubwa ya kufufua uchumi, nikajiuliza nani atafanya mambo ya Kigoma, nikampa Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango mtu wa Kigoma, nikatafuta wa elimu ili ashughulikie na Kigoma, nikamleta Profesa Joyce Ndalichako ni wa  hapa Kasulu, barabara nikamleta Atashasta Nditiye,”alisema Rais Magufuli.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi