loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dodoma Jiji yaikamia Coastal Union

KOCHA msaidizi wa timu ya Dodoma Jiji, Renatus Shija amesema timu yake imejipanga kuifunga Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kesho ugenini uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Akizungumza na gazeti hili jana, Shija alisema vijana wake wapo katika hali nzuri na wamejipanga kushinda. “Coastal Union ni timu nzuri na walishawahi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu.

Wenzetu watakuwa wakipambana kufanya vyema na sisi tutapambana kuhakikisha tunashinda mchezo huo,’’ alisema Shija. Alisema, hakuna mchezaji majeruhi na timu yao ipo katika hali nzuri.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu hasa kwa Dodoma inayotoka ugenini kwa mara ya kwanza ikiikutana na mwenyeji wake aliyetoka kupoteza mechi zote mbili za ugenini.

Katika msimamo wa Ligi Kuu kabla ya mechi za jana, Dodoma Jiji ipo katika nafasi ya Tatu ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi