loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pochettino aiota Real Madrid

KOCHA wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema ndoto yake ni kufundisha Real Madrid siku moja. Pochettino amekuwa nje ya kazi hiyo tangu alipoondoka Spurs Novemba 2019 baada ya kufundisha kwa miaka mitano.

Akiwa Spurs, Pochettino amewahi kuhusishwa na kutembelea Madrid mara kadhaa. “Sijui kama nitawahi tena kuwa kocha wa Real Madrid kwa sababu soka linakupeleka kule linakotaka lakini kwa hakika ni ndoto yangu,” Pochettino aliiambia radio Cadena Cope.

“Kama si bora, basi ni miongoni mwa klabu bora duniani.” “Ina historia nzuri na nadhani siko tofauti na wataalamu wengine kwenye soka yenye weledi.”

“Kila kocha atakuwa ameweka kwenye orodha ya ndoto zake, kuiongoza Real Madrid.” Pochettino, mwenye umri wa miaka 46 alihusishwa na wapinzani wa Madrid, Barcelona mara mbili mwaka huu.

Iliripotiwa alikuwa akipewa nafasi kubwa kumbadili Ernesto Valverde, aliyetimuliwa Januari mwaka huu na alikuwa miongoni mwa wateule wa klabu kwenye kumrithi Quique Setien, aliyeoneshwa mlango wa kutokea baada ya Barca kufungwa mabao 8-2 na Bayern Munich kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa mwezi uliopita kabla ya Barca haijamtangaza Ronald Koeman.

Pochettino, ambaye amecheza na kuifundisha timu mpinzani wa Barca Espanyol mapema katika maisha yake ya ukocha alisema hajapokea ofa yoyote kutoka Barca msimu huu.

“Sijamuona [rais wa Barcelona Josep Maria] Bartomeu lakini nilipata chakula cha mchana na [mtu wa ufundi wa Barcelona] Ramon Planes,” alisema

Pochettino. “Tuna urafiki mzuri lakini sikupewa ofa ya kuwa kocha wa Barcelona.” “Sikupata ofa moja kutoka PSG, au Juventus, au Inter Milan. Nilipata simu kutoka Benfica na Monaco. Sihitaji kudanganya.”

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amejikuta katika wakati mgumu baada ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi