loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

377 wa kaya duni wanufaika Bodi ya Mikopo

WANAFUNZI 377 kutoka kaya duni nchini wamepewa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) baada ya kufaulu masomo yao na kukidhi vigezo vya bodi hiyo.

Hawa ni baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kupitia mpango wa uhamishaji fedha kwa kaya masikini.

Waliandikishwa shule 2014 na walikuwa na mahudhurio mazuri shuleni, ambapo mwaka jana walifaulu vizuri mitihani yao ya Kidato cha Sita na kujiunga na elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini.

Mafanikio haya yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga katika kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu Mpango wa Kunusuru Kata Maskini Awamu ya Kwanza (Tasaf I) -2000-2005 Tasaf II (2005- 2013) na Tasaf III (2013 - 2023) kwa wanahabari 40 kutoka mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya na Njombe kilichofanyika jijini Mbeya.

“Mwaka jana watoto kutoka kaya duni nchini wapatao 377 waliohitimu kidato cha sita na kufaulu mitihani yao ya kitaifa walipewa mikopo na HESLB baada ya kukidhi vigezo haya ni mafanikio makubwa mwaka huu tunatarajia idadi yao itaongezeka maradufu,” alisisitiza.

Mwamanga alisema walengwa wa mpango huo ni kaya masikini zinazoishi katika mazingira duni na hatarishi ambazo zina kipato cha chini sana ambacho si cha uhakika ukilinganisha na nyingine vijijini,mitaani au katika sheria.

Akizungumzia utekelezaji wa Tasaf III, alisema kaya masikini milioni 1.3 zilitambuliwa katika halmashauri zote za Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo kaya maskini milioni 1.1 zenye watu takribani milioni tano ziliandikishwa na asilimia 52 ya walengwa hawa ni wanawake ambapo unatekelezwa katika vijiji, mitaa na shehia 9,986.

“Kiasi cha shilingi bilioni 968.7 zimetumika kwa walengwa wa Mpango mpaka Februari 2020,” alieleza.

Taarifa ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia kuhusu hali ya umasikini Tanzania Bara, inaonesha kuwa bila kuwepo Tasaf, umasikini ungeongezeka kwa asilimia mbili yaani watu milioni moja zaidi wangekuwa masikini na umasikini uliokithiri kuongezeka kutoka asilimia nane hadi 9.2

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mbeya

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi