loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF iwawajibishe waliokagua viwanja vyote vilivyofungiwa

WAKATI Ligi Kuu soka Tanzania Bara ikiwa ndio kwanza ipo raundi ya pili, kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na ubora wa baadhi ya viwanja ambavyo vinatumika katika michezo mbalimbali ya ligi hiyo.

Viwanja hivyo ni pamoja na Gwambina uliopo Misungwi, Mwanza, Karume uliopo Musoma mkoani Mara na vingine.

Ubovu wa viwanja hivyo umelalamikiwa na timu ambazo zimevitumia katika michezo hiyo ya awali na wenyeji wao, huku zikidai kushindwa kufanya vema kwa madai ya viwanja hivyo havina ubora unaostahili.

Hizi taarifa za malalamiko ya kuwepo kwa viwanja vibovu ni za kushangaza, kwani kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Ufundi ilituma wawakilishi kwa ajili ya kukagua viwanja hivyo ili kuona kama vinastahili.

Kamati iliridhika na ubora wa viwanja hivyo na ndio maana ilivipitisha vitumike kuchezea ligi, lakini maajabu baada ya michezo kadhaa kupigwa imebainika kwamba havina ubora.

Kwamba, Kamati ya Ufundi iliruhusu kutumika viwanja hivyo kwa kutimiza tu wajibu, huku ikijua fika havina ubora unaostahili? Suala la viwanja si dogo hata kidogo ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo kabla ligi haijasogea hatua zaidi kwani bila hivyo kunaweza kutokea mambo mengine, ambayo yatakuja kutibua kabisa mwelekeo wa Ligi.

Pamoja na kwamba viwanja hivyo vimeshafungiwa, lakini wahusika ambao walitumwa kuvikagua na kuvipitisha nao wanatakiwa kuwajibishwa kwasababu walichokifanya ni uzembe usio vumilika.

Kwasababu ikumbuke mjumbe au wajumbe waliotumwa kukagua walilipwa posho na TFF, kwa ajili ya safari ina maana hizo pesa zimekwenda bure maana kazi waliyotumwa wameshindwa kuitimiza.

Nafikiria ndani ya shirikisho hilo kuna watu bado hawana nia njema na soka la Tanzania na lengo lao bado liko katika maslahi binafsi na ndio maana wanafanya madudu kama haya.

Wiki iliyopita ambayo ndio mechi za mzunguko wa kwanza zilianza, tuliona waamuzi walivyoboronga lakini wiki ya pili viwanja navyo vinatia doa hili halivumiliki wahusika wanapaswa kuwawajibisha wote waliohusika ili kuongeza weledi katika usimamizi wa mpira wetu.

Imepenya inafahamu kwamba mbali na viwanja vya Gwambina na Karume vipo viwanja vingine bado havikizi vigezo vya kuchezewa mechi za ligi na kinachofanywa hivi sasa ni siasa ili kuficha madhambi ya wajumbe waliotumwa kwa maslahi yao binfsi.

Viwanja kama vya Mkwakwani na Nelson Mandela vipo kwenye orodha ya vitakavyo tumika kucheza ligi ya msimu huu, lakini kiukweli viwanja hivyo vinakosa sifa katika baadhi ya maeneo ikiwepo vyumba vya kubadilishia nguo na sehemu ya kuchezea.

Lakini siasa zetu za lazima timu ya mkoa fulani icheze kwenye uwanja wa nyumbani hata kama hauna sifa ndio zinapelekea haya yote ya viwanja kupitishwa hata kama havina sifa, sasa hivi hatujengi bali tunabomoa.

Zipo baadhi ya timu zimeingia gharama kubwa kusajili wachezaji wazuri kutoka nje ya nchi lengo mbali na ubingwa lakini kuona burudani ya namna soka la ufundi linavyo chezwa, lakini kwa ubovu wa viwanja hivyo hakuna lolote cha zaidi wachezaji hawa watakuwa wakionekana wakishaini Benjamini Mkapa, Kaitaba na Nyamagana tu.

Ifike wakati TFF iwe makini na kile ilicho kikusudia soka ni mchezo wenye mashabiki wengi nchini inapaswa kulitambua hilo na kuweka miundombinu mizuri ili kuzidi kuwavutia wawekezaji na hata wachezaji wakigeni waweze kuja kwa wingi, vinginevyo tutabaki na akina Ngassa na Boban wetu kila siku.

MILA na desturi ni muhimu katika mustakabali wa malezi ya ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi