loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wolves ‘ya Wareno’ ndani ya EPL

KATIKA jumla ya klabu 20 za Ligi Kuu England (EPL) msimu huu ipo pia Wolverhampton Wanderers Football Club maarufu kama Wolves.

Klabu hii ambayo ilianzishwa kwa jina la ST Luke’s FC mwaka 1877, inapatikana katika eneo la Wolverhampton, Magharibi mwa Midlands, England.

Ilipanda EPL msimu wa 2017/18 baada ya kuwa mabingwa wa Championiship, kwenye misimu yao yote miwili 2018/19 na 2019/20 wamemaliza kwenye nafasi ya saba.

Klabu hii imepata mafanikio makubwa ndani ya misimu yake miwili kwenye EPL ambapo msimu uliopita kwenye Michuano ya Europa League walifika nusu fainali ikiwa ni mara yao ya kwanza klabu hiyo kushiriki michuano ya Ulaya baada ya kupita miaka 39.

Kwa sasa inanolewa na kocha ‘mbishi wa timu vigogo’ Nuno Herlander Simoes Espirito Santo raia wa Ureno aliyezaliwa Januari 25, 1974.

Amewahi kucheza soka na alikuwa akiimudu nafasi ya mlinda mlango na alijumusihwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa Ureno kilichoshiriki Euro 2008, katika kipindi chote alichoitumikia timu ya taifa hakuwahi kupata kombe lolote.

Maisha yake ya ukocha yalianzia katika Klabu ya Panathinaikos akiwa kocha msaidizi na ilipofika mwaka 2012 alikabidhiwa jukumu la kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu hiyo.

Bada ya hapo akahamia akaamua kurudi kwao Ureno na akapata kibarua kwenye timu ya Rio Ave ambayo ilinyakua mataji mawili nadani ya mwaka mmoja, 2014, baadae akapata dili la kwenda Hispania kuinoa Klabu ya Valencia.

Wolves ipo England lakini kwenye wachezaji wake 30, watano tu ndio Waingereza huku Wareno wakiwa ndio na idadi kubwa. England ni tofauti na Tanzania ambapo kuna sheria ya kuchunga idadi ya wachezaji wakigeni kusajiliwa kwenye timu moha.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linazitaka klabu kusajili wachezaji wakigeni wasiozidi 10 lakini kwa Chama cha Soka England (FA) wao wamezipa ruhusa klabu kusajili idadi yoyote ya wachezaji wakigeni wanaowahitaji.

Licha ya kuwa mashirikisho mengi hayana kiwango maalumu cha wachezaji wakigeni lakini ni mara chache kuona klabu ya nchi husika kuwa na wageni wengi kutoka nchi moja kuliko wazawa.

Wareno kwenye timu ya Wolves wapo 12, wachezaji 11 na kocha mmoja, kati ya hao wachezaji 10 wapo kikosini kwa sasa, mmoja ametolewa kwa mkopo.

Kwa idadi hiyo hapo inahesabika ni sawa na kikosi cha kwanza cha Wareno kikiwa na kocha wao Mreno kikacheza kwenye EPL. Wachezaji hao ni Pedro Neto, Ruben Neves, Jose Moutinho, Ruben Vinagre, Daniel Podence, Rui Patricio, Fabio Silva, Roderick, Diogo Jota,

MILA na desturi ni muhimu katika mustakabali wa malezi ya ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi