loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Onyango, Calinhos Waanza kujenga ufalme

I MEKUWA ni kawaida ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupata wachezaji wapya kutoka mataifa mbailimbali kila msimu unapoanza au katikati ya msimu dirisha dogo limapofunguliwa.

Klabu hutumia kila mbinu kuhakikisha wanachukua wachezaji hao ili kutoa mchango wao katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi, Kombe la FA pamoja na michuano ya kimataifa kama itakuwa inashiriki.

Kwenye harakati za kusajili umakini mkubwa hufanyika, mambo huwa ya siri ili kuepuka kuzidiana keti na klabu nyingine. Licha ya mikakati yote mpaka kufikia hatua ya kumnasa mchezaji, lakini mara kadhaa hutokea baadhi ya wachezaji hao kushindwa kufanya kile klabu inachokitarajia hatimaye kujikuta ikiingia kwenye mzigo wa kuwalipa mishahara bila kutoa manufaa.

Katika msimu huu zaidi ya wachezaji 10 wapya wakigeni wamesajiliwa, lakini ndani ya mechi mbili ni wachezaji watano tu ndio wameanza kuonesha makali yao na kuanza kukaa vinywa ni mwa mashabiki wa klabu zao.

Tangu ligi ilipoanza Septemba 6, mwaka huu kila timu imeshacheza mechi mbili, msimamo unaonesha walioshika nafasi za juu KMC ndio vinara wa ligi, wakifuatiwa na Azam FC, Dodoma Jiji na Biashara United wakati Simba SC inashika nafasi ya tano huku nafasi ya sita ipo Yanga.

Kwenye mechi hizo kumeonesha wazi wachezaji ambao haraka wameanza kuonesha makali yao na kama ilivyokuwa kawaida ya mashabiki kumpenda mchezaji anayeonesha uwezo uwanjani wameanza kutajwatajwa kila wakati.

JJOASH ONYANGO

Klabu ya Simba mwaka 2018 walimsajili Meddie Kagere kutoka Gor Mahia na akawapa mafanikio, mwaka jana pia wakaenda katika klabu hiyo kumsajili Francis Kahata.

Mwaka huu hawakutaka upite hivi hivi walibisha hodi klabuni hapo kutaka saini ya beki wa kati, Joash Onyango mwenye umri wa miaka 27.

Onyango alikuwa anajua akifika Simba kupata namba lazima afanye kazi ya ziadi kutokana na uwepo wa mabeki wengi wakati ambao walikuwepo msimu uliopita, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Kenedy Juma na Ibrahim Ame ambaye alisajiliwa msimu huu.

Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck amempa nafasi na katika dakika zote alizocheza amewaonesha wana Simba kuwa hakuja kupoteza muda bali ana kazi maalumu ya kuhakikisha washambuliaji wa timu pinzani hawaipenyi ngome ya ulinzi ya Simba na kufunga mabao.

Uwezo wake umewafanya mashabiki na wapenzi wa Simba kutokuwa na mashaka naye wanapomuona kwenye orodha ya wachezaji wanaoanza kwenye mechi husika.

Onyango sio beki wa mchezo mchezo kazi kubwa anayoifanya uwanjani msimu wa 2018/2019 aliibuka kuwa mchezaji bora pamoja na beki bora wa msimu katika Ligi Kuu Kenya.

Onyango ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, alipata tuzo hiyo kutoka kwa muungano wa wanahabari wa michezo Kenya (SJAK), ambayo huitoa kila mwaka.

CARLOS CARLINHOS

Dakika 29 alizopewa na Kocha Zlatko Krmpotic kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City zilimtosha kabisa kuonesha kile kilichomo mguuni mwake na akilini mwake.

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo majina yake kamili ni Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo ‘Carlinhos’ amesajiliwa na Yanga akitokea Interclube ya Luanda, Angola.

Mambo aliyoyaonesha uwanjani ni balaa tupu, ana kasi, fundi wa kukaa na mpira kwa muda mrefu bila kupokonya, ana uwezo wa hali ya juu wa kupokea pasi na kupiga pasi zenye macho, kubwa zaidi ni mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa pamoja na kupiga mashuti ya mbali.

Mpira wake wa kona dakika ya 86 uliotua kichwani mwa Lamine Moro ndio uliozaa bao pekee katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kushinda kwa mbinde 1-0.

Mechi ya kwanza dhidi ya Tanzania Prisons iliyomalizika kwa sare ya 1-1 hakucheza, lakini kiwango chake ndani ya dakika hizo 29 kila shabiki sasa anamjua Carlinhos ni nani.

PRINCE DUBE

Huko Azam huwaambii kitu kuhusu mshambuliaji wao mpya raia wa Zimbabwe, Prince Dube ambaye katika mabao matatu ya klabu hiyo, mawili ameyafunga yeye.

Dube ambaye amesajiliwa kutoka Klabu ya Highlanders FC ya Bulawayo, Zimbabwe nii mmoja ya washambuliaji hatari kwenye Ligi Kuu ya Zimbabwe, ni mmoja ya wachezaji waliokuwa wanaunda kikosi cha timu yake ya taifa kwenye mechi zinazohusisha wachezaji wa ligi ya ndani.

Benchi la ufundi la Azam FC linaloongozwa na kocha mkuu, Aristica Cioaba, limeridhishwa na kiwango chake, ambapo amemuanzisha katika mechi zote mbili.

Dube ni mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu katika kutafuta bao, ukizubaa anaweza kukufunga muda wowote iwe kwa kichwa, mguu wa kulia au kushoto, kikubwa ahakikishe mpira unaingia wavuni.

Kwa misimu ya hivi karibuni Azam imekuwa ikisajili washambuliaji wa kimataifa lakini hawadumu, viwango vyao huonekana ni duni mpaka kufikia hatua ya uongozi kuamua kuvunja mikataba yao, lakini kwa Dube bila shaka wamepata kile walichokuwa wakihitaji.

MICHAEL SARPONG

Sidhani kama kuna mtu asiyeufahamu uwezo mkubwa wa mshambuliaji huyu raia wa Ghana, Michael Sarpong. Yanga wamemsajili Sarpong kuziba pengo la mfungaji bora kwa klabu hiyo msimu uliopita, David Molinga.

Katika dakika alizocheza ndani ya mechi mbili zimedhihirisha uwezo mkubwa aliokuwa nao, kiasi mpaka mashabiki wamekuwa wakimtaja kila wanapozungumza kuhusu Yanga.

Mshambuliaji huyo ambaye ili kumkaba anahitajika apatikane beki mwenye uwezo wa hali ya juu ambaye atatakiwa kuacha kufikiria mambo mengine, akili yake yote aielekeze kwa Sarpong.

Hata kama atazuia asifunge bao, lakini huwa ni ngumu kuzuiwa asifanye makeke yake uwanjani. Kwenye mechi mbili alizocheza amefunga bao moja wakati Yanga ilipotoka sare ya bao 1-1 walipocheza dhidi ya Tanzania Prisons.

INASIMULIWA kuwa miaka takribani 1000 iliyopita, eneo hili Ugogo ambalo ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi