loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nani ni nani Ligi Kuu England 2020-21?

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya England 2020/2021 umeanza na wengi wanajiuliza nani atamaliza katika nafasi gani mwishoni mwa msimu huu utakapomalizika?

Msimu mpya ulianza siku 48 tu baada ya kumalizika ule uliopita, huku Liverpool ikitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 tangu ilipolitwaa taji hilo kwa mara ya mwisho.

Wengi wanajiuliza kama kweli kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na wachezaji wake wanaweza kurudia makali yao ya msimu uliopita? Bado klabu zinaendelea kukamilisha usajili ili kuimarisha vikosi vyao kabla ya dirisha halijafungwa.

1. Liverpool

Msimu uliopita ilimaliza ya kwanza Klabu hii ina kibarua kigumu kutetea taji lake, ambapo kwanza ilishinda taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya misimu miwili iliyopita, lakini ni timu ambayo inaonekana kutokuwa na udhaifu wowote imesheheni wachezaji muhimu katika kila idara.

Klopp hadi sasa bado hajafanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha usajili baada ya kulipa kiasi cha Pauni milioni 11 kumsajili Kostas Tsimikas lakini jina la mchezaji wa Bayern Munich, Thiago Alcantara bado linahusishwa na jina hilo.

Pamoja na ubora wake, lakini bado ni ngumu kutetea tena taji hilo la Ligi Kuu ingawa ina nguvu na uwezo wa kufanya hivyo. Ubingwa tena-lakini msimu huu mbio za ubingwa zitakuwa karibu sana.

2. Manchester City

Msimu uliopita ilikuwa ya pili Manchester City ni timu yenye beki dhaifu sana, hivyo ilikuwa vigumu kwao kushinda taji msimu uliopita. Imefungwa mara tisa.

Kushindwa kumbadili beki wao aliyeondoka Vincent Kompany ndani na nje ya uwanja limekuwa ni kosa kubwa.

Pep Guardiola amejaribu kuziba pengo hilo kwa kumsajili Nathan Ake kutoka Bournemouth kwa ada ya Pauni milioni 41 na wanahusishwa na mchezaji wa Napoli Kalidou Koulibaly, ambaye hata hivyo wanasema haendi kokote, pamoja na mshambuliaji wa Valencia Ferran Torres naye pia yuko katika rada zao.

Phil Foden ndio atakuwa tegemeo katika safu yao ya ulindi, ingawa watakosa huduma ya David Silva. 3.

CHELSEA

Msimu uliopita ilimaliza ya nne Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amemwaga fedha kama alivyokuwa akifanya huko nyuma, lakini bila kusahau kuwa klabu nayo ina fedha za kutumia zilizotokana na mauzo ya baadhi ya nyota wake kama akina Eden Hazard na Alvaro Morata.

Timu hii katika dirisha kubwa la usajili imefanya kweli kwa kusajili wachezaji kibao wakiwemo wawili chipukizi wa Kijerumani, Timo Werner na Kai Havertz ambao wameungana na beki wa England, Ben Chilwell anayetokea Leicester City pamoja na Mbrazil mzoefu Thiago Silva.

Inaonesha jinsi gani kocha wao, Lampard amejaribu kutumia rasilimali iliyopo kutatua matatizo ya upande wa kipa Kepa Arrizabalaga, ambaye amepoteza imani ya kocha wake msimu uliopita.

Edouard Mendy wa Rennes sasa ndio anaonekana kupewa kazi hiyo ya kuzuia mipira isiingie nyavuni. Sio washindi wa taji lakini wanaweza kutwaa kombe.

Hiyo itatosha kwa mmiliki kwa klabu hiyo, Abramovich, ambaye anatarajia marejesho kutoka katika kile alichokiwekeza.

4. Manchester United

Msimu uliopita ilimaliza ya tatu Imejiimarisha kiasi baada ya kumsajili Bruno Fernandes, ambaye anaiweka Manchester United katika nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa pale ligi itakapomalizika, na kuwasili kwa Donny van de Beek kutoka Ajax kumeingezea nguvu timu hiyo kwa upande wa kiungo.

United iko vizuri sehemu ya ushambuliaji, lakini bado imemuongeza mchezaji wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho lakini kushindwa mara tatu katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita, kumeweka wazi udhaifu wao, na David de Gea ataongeza kiwango pamoja na Dean Henderson ambaye amerejea akitokea Sheffield United? Timu hiyo inatarajiwa tena kuwemo katika nne bora msimu huu, lakini kimakali bado hawajawakaribia mabingwa Liverpool.

5. Tottenham

Msimu uliopita ilikuwa ya sita Jose Mourinho imeiimarisha Spurs msimu uliopita na ameongeza wakali wawili, Pierre-Emile Hojbjerg na Matt Doherty ili kuiongezea nguvu zaidi safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Harry Kane na Heung-Min Son.

Hatahivyo, kocha huyo itabidi kupambana kweli kweli ili kuweza kumaliza ndani ya nne bora, lakini pia itataka kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.

6. Arsenal

Msimu uliopita ilimaliza ya nane Kocha Mikel Arteta kutwaa taji la FA mwishoni mwa msimu wake wa kwanza wa kuifundisha timu hiyo, ni jambo kubwa na kumemfanya kuzidi kujiamini zaidi.

Timu hiyo sasa inaonesha kuwa inaweza kuzisambaratisha Liverpool, Manchester City na Chelsea. Katika kikosi chake ameongeza wachezaji wazoefu pamoja na wenye ujuzi mkuwa kama akina Willian kutoka Chelsea wakati Gabriel Magalhaes, alisajiliwa kutoka klabu ya Lille, ni mmoja wa mabeki mahiri kabisa barani Ulaya.

Arteta pia atataka kuongeza wachezaji katika kikosi chake kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, huku akimuongezea mkataba nahodha wake, PierreEmerick Aubameyang.

Kocha huyo atataka kuongeza mataji katika kabati la klabu hiyo kwa kutwaa taji la Ligi ya Ulaya. Sasa kunafanya utabiri kuwa mgumu sana kwa timu hiyo.

7. Everton

Msimu uliopita ilikuwa ya 12 Kiasi kuna imani zaidi kwa kocha Carlo Ancelotti , lakini uwezo wake wa kuwavutia wachezaji na rekodi yake ya mafanikio ina maana kuwa ataiimarisha zaidi Everton msimu huu.

Ancelotti amejenga sehemu ya kiungo, ambapo amewaongeza Mbrazil Allan na Abdoulaye Doucoure kutoka Watford, wakati kuwasili kwa James Rodriguez kutoka Real Madrid kumeongeza uimara wa kikosi chake.

8. Wolverhampton Wanderers

Msimu uliopita ilikuwa ya saba Wolves ilikuwa na msimu mzuri nyumbani na ugenini, lakini ilionekana kuchoka wakati msimu wao mzuri wa Ligi ya Ulaya ulipomalizika katika hatua ya robo fainali walipofungwa dhidi ya mabingwa Sevilla. Nafikiri Wolves watashindania tena kucheza Ligi ya Ulaya.

9. Leicester City

Msimu uliopita ilikuwa ya tano Leicester City iliyomaliza katika nafasi ya tano inachukuliwa kama ilipata mafanikio, lakini ilikatishwa tamaa na kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, licha ya msimu mzima kuwa ndani ya nne bora.

Jamie Vardy ndiye aliyebaki kama jembe la timu hiyo wakati beki Ben Chilwell amekwenda Chelsea, ambapo timu hiyo itawekeza katika ubunifu wa James Maddison kuisaidia timu hiyo kuvutia na kuwa kikosi hatari chini ya kocha Brendan Rodgers.

10. Southampton

Msimu uliopita ilikuwa ya 11 Mashabiki wa Southampton bado wana kumbukumbu mbaya ya timu yao kufungwa 9-0 nyumbani dhidi ya Leicester City Oktoba mwaka jana, lakini wanakumbuka pia jinsi kocha Ralph Hasenhuttl na wachezaji wake walipobadilisha msimu na kumaliza katika nafasi ya 11.

Timu hiyo inayojulikana kama Watakatifu wanacheza kwa nguvu sana, hasa wanapokuwa nje ya nyumbani kwao na Danny Ings ana washambuliaji bora kabisa katika Ligi Kuu ya England, wamefunga mabao 22 msimu uliopita.

Kyle Walker-Peters amesajiliwa kutoka Spurs, ingawa Pierre-Emile Hojbjerg ni pigo kubwa kumpoteza. Nafikiri Watakatifu hao walikuwa na msimu mzuri sana.

 

Itaendelea wiki ijayo.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi