loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘JPM amefanya makubwa, apewe miaka 5 mingine’

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais John Magufuli amefanya makubwa na anastahili apewe miaka mitano mingine, akamilishe kazi nzuri aliyoianzisha.

Pia, amewataka Watanzania waweke kando itikadi zao za vyama na wamchague Rais Magufuli kwa sababu maendeleo hayachagui chama.

Alitoa mwito huo juzi wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Lagangabilili wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kwenye mkutano wa kampeni, uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Lagangabilili.

Akielezea yaliyofanyika chini ya Ilani ya CCM kwenye sekta ya miundombinu, Majaliwa alisema Sh bilioni 3.2 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara ikiwemo barabara za kutoka Chinamili-Nanga; BudalabujigaMitobo-Nguno; Lagangabilili-Migato-Ndoleleji na Inalo-MahembeSawida.

Kuhusu elimu, alisema Sh bilioni 1.87 zilitolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya nyumba za walimu, vyoo na madarasa kwa shule za msingi ikiwemo shule za Ngeme, Mahembe, Sawida A, Gambasingu ‘A’, Kidula, Mlimani, na Ikindilo.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi