loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tembo aua mtu Arusha

TEMBO wameingia katika makazi ya watu katika jiji la Arusha eneo la Njiro kata ya Engutoto na kusababisha kifo cha mtu mmoja, aliyetaka kumpiga picha tembo akiwa juu ya mti.

Ofisa wa Kikosi cha Ujangili Kanda ya Kaskazini (KDU), Michael Msokwa alithibitisha tukio la tembo kuingia mjini na kuua mtu, ambaye hajatambuliwa jina lake mpaka sasa.

Msokwa alisema kuwa mtu huyo aliuawa na tembo huyo aliyetokea katika mbuga za wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Mtu huyo alikwenda karibu na mti ulio karibu na mnyama huyo na kupanda juu, kwa lengo la kutaka kumpiga picha kupitia simu yake ya kiganjani.

Alisema baada ya tembo kumuona mtu huyo, alimfuata na kumteremsha kwa kutumia mkonga wake na kisha kumkanyagakanyaga hadi kufa.

Ofisa huyo ambaye ni Mwendesha Mashtaka wa KDU Kanda ya Kaska- zini, alisema kuwa hivi sasa wanafanya utara- tibu wa kumrudisha mnyama huyo katika eneo alikotoka au katika mbuga ya Tarangire yenye tembo wengi.

“Tunafanya utaratibu wa kumrudisha mbugani, aidha mbuga ya Tarangire inayoongoza kuwa na tembo wengi, au kule alikotokea katika mbuga za Simanjiro ambayo ziko karibu na mbuga hiyo,” alisema Msokwa.

Kuonekana kwa tembo huyo huko Msolwa Njiro, kulizua taharuki kwa wananchi wa eneo hilo, ambapo baadhi walijificha majumbani na kutafuta mawasiliano ya maofisa wanyamapori mkoani Arusha ili wamuondoe.

Wengine walitafuta namna ya kumpiga picha. Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Athumani Mfaume alisema kuwa jamii inapaswa kujifunza namna ya kujikinga na wanyama wakali wanapovamia makazi yao.

Alisema mtu aliyeuawa alifanya masihara na mnyama huyo, kwa kuamua kutaka kumpiga picha wakati akiwa juu ya mti ambao si mrefu, na matokeo yake amehatarisha maisha yake mwenyewe.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi