loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtoto wa Turky ashinda kura za maoni ubunge

MTOTO wa aliyekuwa mgombea wa jimbo la Mpendae, Salim Turky aliyefariki dunia hivi karibuni , Toufiq Salim Turky (40) ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za kupata mgombea ubunge katika jimbo hilo.

 Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar,  Catherine Nao akizungumza na gazeti hili jana,  alisema mchakato huo ulihusisha wagombea 14,  ambao walikuwa na nia ya kurithi nafasi ya marehemu Turky.

Alisema Toufiq alipata kura 33 sawa na aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la Paje, ambaye pia alikuwa mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia nafasi tano za kutoka Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub aliyepata kura 33.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) ambaye pia alikuwa Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Juma Khamis alijitoa katika kinyanganyiro katika hatua za awali.

Miongoni walioanguka katika kinyanganyiro hicho ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Omar Said Ameir.

''Nimeshiriki katika mchakato huo lakini kura hazikutosha...hata hivyo lengo letu kubwa ni kuona tunapata mgombea mwenye uwezo atakayepeperusha bendera ya chama na kuona CCM kinaibuka na ushindi wa kishindo''alisema Ameir .

Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa CCM,  majina ya wagombea hao yatafikishwa katika kikao cha Kamati Maalumu ya CCM kitakachofanyika leo, kwa ajili ya kufanya uteuzi wa jina la mgombea mmoja, atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28''alisema.

''Kamati Maalumu ya Halmashauri  Kuu ya CCM Zanzibar itakutana kesho (leo) kwa niaba ya Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kufanya uteuzi wa jina la mgombea mmoja atakayepewa jukumu la kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa jimbo la Mpendae''alisema.

Toufiq ni mtoto wa kwanza wa marehemu Turky. Kwa sasa Toufiq ni rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda ya Zanzibar. 

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Khatibu Suleiman, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi