loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli: Ndege siyo anasa

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ameelezea ununuzi wa ndege unavyomnufaisha Mtanzania moja kwa moja akisisitiza kuwa ndege si anasa, tofauti na inavyodaiwa na baadhi ya watu alioita kuwa wana mawazo yaliyopotoka.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli aliyoitoa jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Lake Tanganyika, mkoani Kigoma, imeungwa mkono na watu wa kada tofauti, wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na wasomi, ambao wameeleza faida ambazo nchi inapata kwa kumiliki ndege.

Aidha, takwimu za serikali zinaonesha faida zilizopatikana baada ya serikali kuboresha usafiri wa anga kwa kununua ndege zake miongoni mwa faida ikiwa ni upatikanaji ajira na mapato kupitia kodi.

 Ndege si anasa

Akihutubia maelfu ya watu mjini Kigoma jana, Rais Magufuli alisema  ndege zina faida katika maendeleo, kwani pamoja na kutumika kama usafiri, lakini pia zinachangia katika uchumi kwa kutengeneza ajira na kuvutia utalii.

Alisema utalii ni sekta inayoajiri watu wengi, ambayo katika miaka mitano imeajiri watu milioni nne.

“Hata hizi ndege zimetengeneza ajira, wale walioajiriwa kwenye ndege marubani na mainjinia (wahandisi) wameajiriwa zaidi ya 500, hebu fikirieni ndugu zao na familia zao wamenufaikaje na ndiyo maana tumepanga kuendelea kununua ndege zaidi,” alisema.

Alisema nchi zenye ndege zake, ndio zinaongoza kwa kuwa na watalii wengi duniani ikiwemo nchi ya Morocco na Misri. “Ndio maana sisi hatuwezi kubaki nyuma, ukinunua ndege unaambiwa eti ni luxury (anasa), haya ni mawazo yaliyopotoka,” alisema.

Alisema tayari awamu ya kwanza ya miaka mitano, serikali imenunua ndege 11, ambazo nane zimewasili na tatu hazijawasili. Vile vile serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine tano awamu ya pili ya miaka mitano.

Akielezea zaidi faida za ndege, alisema serikali inapopeleka dawa kwenye mikoa kwa ajili ya hospitali haitumii magari, bali hutumia ndege ili zifike haraka. “Wale wagonjwa wanaotumia hizo dawa leo watasema ndege zisije?

“Nimefurahi nilikuwa naonyeshwa picha, nyinyi wajanja kweli watu hapa (Kigoma), picha inamuonesha Zitto anateremka kwenye ndege bombardier, nikasema kweli maendeleo hayana chama, hata waliopinga ndege kumbe wanapanda. Nyie wajanja, hii mlipanga kunionesha mimi, singemuonesha mwenyewe?,” alisema.

Wachambuzi wanena

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mbunda alisema mjadala unaoendelea katika majukwaa ya kampeni kuhusu maendeleo yaliyopo nchini, kwamba ni ya vitu na si watu, ni wa kisiasa usio na mantiki.

Alieleza kuwa miradi mingi ya kimkakati ya serikali, lazima ilenge msingi mzima wa ukuaji uchumi. “Rais anapotangaza kujenga Tanzania ya viwanda lazima aboreshe umeme na miundombinu ambapo suala la anga linaingia,” alisema.

Alisema endapo uwapo wa shirika la ndege pamoja na ununuzi wa ndege, usingekuwa na mchango katika uchumi, ni wazi kuwa Rais Magufuli asingehangaika kulifufua shirika hilo, lakini kutokana na umuhimu wake hususani katika utalii amelifufua.

“Sisi tuna vivutio vingi vya utalii na hifadhi za taifa, tunapokea wageni sana, huwezi kuwa na sekta ya utalii kamilifu kama hauna shirika la ndege. Ni kweli wananchi wanaweza wasipande hizo ndege lakini kupitia mapato yanayopatikana huduma wanazopata za afya, elimu bure, umeme na maji zilizoboreshwa na mapato hayo moja kwa moja wananufaika,” alieleza.

Mwanasiasa aliyewahi kuwa mbunge wa upinzani, David Kafulila alibainisha kuwa uwapo wa ndege nchini ni jambo muhimu la kiuchumi, kutokana na ukweli kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwa utalii Afrika na ya pili duniani.

“Katika Bunge la 10 la mwaka 2010 hadi 2015, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 60 ya watalii nchini wanatumia usafiri wa anga hivyo kuna umuhimu kama nchi kuwa na ndege,” alieleza.

Alisema pia katika Ripoti ya Umasikini na Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2008, ilionesha kuwa sekta ya anga ni moja ya maeneo muhimu katika suala zima la kukuza uchumi wa nchi.

“Kutokana na hali hii ni wazi kuwa uwepo wa ndege una umuhimu mkubwa pamoja na kuvutia watalii, lakini pia unaipatia nchi fedha za kigeni zitakazotumika katika shughuli nyingine za maendeleo,” alieleza Kafulila.

Kafulila alieleza anavyoshangazwa na vyama vya siasa ambavyo kwa sasa vinapinga ununuzi wa ndege wakati katika mabunge yote yaliyoongozwa na Spika Pius Msekwa, Samuel Sitta na Anne Makinda, hoja kubwa bungeni ilikuwa ni kwa nini serikali haina ndege zake.

“Hii hoja imeanza muda mrefu. Kila Bunge walikuwa wakihoji kwa nini nchi kama Tanzania iliyo na nafasi nzuri kijiografia haina ndege zake na kuitolea mfano nchi ya Rwanda,” alisema.

Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, alionesha kuchukizwa na namna baadhi ya wapinzani, wanavyopotosha kuwa hakuna nchi duniani inayomiliki ndege, jambo ambalo si la kweli.

“Mimi nawaambia zipo nchi zinamiliki ndege zake na zinafanya vizuri kiuchumi. Nendeni google katafuteni shirika la ndege la Egypt Airline na Ethiopia Airline zinamilikiwa na nani? Zote serikali zake zinamiliki mashirika hayo kwa asilimia 100,” alisisitiza.

Kitakwimu, taarifa za serikali zinaonesha maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya usafiri wa anga , yamefanikisha ongezeko la idadi ya abiria kutoka 5,600 kwa mwezi hadi 65,000 kwa mwezi.

Mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni  2.5 kwa mwezi hadi Sh 15 bilioni kwa mwezi. Kodi inayopelekwa serikalini imeongezeka kutoka Sh milioni 103  hadi Sh bilioni 1.25. Vile vile jumla ya malipo serikalini ya tozo ya ukodishaji ndege ni Dola za Marekani milioni 15.4 milioni.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi