loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ghasia: CCM imefanya makubwa, azindua kampeni

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, kwa tiketi ya CCM  Hawa Ghasia, amezindua kampeni za uchanguzi katika jimbo hilo huku akiwataka wananchi kupuuza watu wanaoeneza uongo kuwa CCM imeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Mkunwa jimboni hapo, Ghasia amesema CCM imefanya mambo makubwa ikiwemo kujenga miradi mingi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Alitaja baadhi ya miradi iliyojengwa na mingine kuboreshwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari 10 ambazo mbili  kati ya hizo zimekamilika na kuanza kuchukua wanafunzi.

Pia  shule nyingine ziko katika hatua ya kukamilika na kwamba hadi kufikia Januari mwakani zitaanza kuchukua wanafunzi.

Ametaja shule mpya ni  Kitere, Cheleni, Liquid, Mangopachanne, Msangamkuu, Sinde, Tangazo, Mbawara na Muungano.

Aidha amesema ujenzi wa shule hizo umeenda sambasamba na ujenzi wa mabweni Kisiwani  na Sekondari ya Libobe na kwamba jimbo hilo pia limeshapata hela kutoka serikani kwa ajiili ya kuanza ujenzi wa mabweni mengine katika shule ya Kitere na Nanguruwe.

Afya:

Kwa upenda wa afya, Ghasia amesema serikali imejenga hospitali ya wilaya na vituo vya afya kikiwemo Kilambo, Mkunwa na Mahurunga.

“Pia tunaendelea na ujenzi wa vituo vingine vya afya na zahanati kuhakikisha kila mwananchi katika kijiji chake anapata huduma za afya bora,” amesema.

Barabara:

Mgombea huyo amesema  CCM kupitia serikali yake iliweza kujenga na kuboresha barabara za ndani ya jimbo hilo zikiwemo zile zinazounganisha wilaya ya Mtwara vijijini na wilaya zingine.

“Barabara ndani ya jimbo letu zimejengwa na kuboreshwa, mda wote zinapitika na hata kutumiwa na viongozi wengine, hupita wakienda katika maeneo yao,” amesema.

Umeme:

Kwa upande wa umeme vijijini, Ghasia amesema zaidi ya vijiji 80 vimeunganishwa na umeme kati  ya vijiji 110 na kwamba hadi kufika mwezi wa sita mwakani, vijijini vyote vitaunganishiwa umeme.

Maji:

Ametaja miradi ya maji ambayo pia CCM imejenga na kufanikisha upatikanaji wa maji kwa asilimia kubwa.

Amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchangua mgombe uraisi wa CCM John Magufuli ili aweze kuendeleza na kukamilisha miradi mingi ambayo ameanzisha na mingine ambayo anatarajia kuanzisha,

foto
Mwandishi: ANNE ROBI Mtwara

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi