loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake acheni imani potofu kuhusu ugonjwa wa selimundu

MWANAMKE unapojifungua ni vema ukahakikisha afya ya mtoto wako kwa kumpima afya yake vizuri, lakini kuna wakati baadhi ya wanawake wamekuwa wakisahau kushirikiana na akinababa kupima watoto wao wanapopimwa ugonjwa wa selimundu.

Mwezi huu ni mwezi maalumu wa kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo maarufu ‘sickle cell’ ambao umekuwa ukiongezeka nchini kila kukicha kutokana wa watoto kuzaliwa wakiwa na ugonjwa huo.

Hivyo ni vyema wanawake wanapojifungua wahakikishe mtoto anafanyiwa kipimo hicho hususan pale mtoto unapomuona anakabiliwa na matatizo mbalimbali ya afya kwani ugonjwa huo huathiri seli nyekundu.

Inaelezwa kuwa vifo vingi vya watoto wenye selimundu hutokea kutokana na wazazi kuwa na uelewa mdogo kuhusu ugonjwa huo na kukosekana kwa huduma za utambuzi hivyo ni vema kupata elimu stahiki.

Kutokana na ukosefu wa elimu kuhusu ugonjwa huo, zimekuwepo imani potofu ikiwemo kuwa watoto wanaougua ugonjwa huo hawafikishi miaka 18, jambo ambalo si kweli kwani mtoto akibainika mapema anaweza kupatiwa matibabu stahili.

Inaelezwa kuwa kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa nchini, wa nane huzaliwa wakiwa na ugonjwa huo na kuwa asilimia 6.7 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano huchangiwa na ugonjwa huo, kutokana na wengi wao kutotambua watoto wao wana ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi zinazojihusisha na ugonjwa huo wa selimundu Tanzania -TANSCDA, Dk Deogratius Soka anabainisha kuwa kaulimbiu ya mwaka huu ni “Ijue Selimundu, Ondoa Unyanyapaa.”

Kwani ukiujua ugonjwa huu itakuwa rahisi kupambana nao. Alifafanua kwamba, watoto wenye selimundu wakiwahi kufikishwa hospitali wakapatiwa vipimo sahihi na tatizo kubainika mapema, kisha kupatiwa tiba sahihi, wanaweza kuishi zaidi ya miaka 18 kwani wapo wenye umri mpaka miaka 60 wakiishi na ugonjwa huo, ikiwemo madaktari, wauguzi na watendaji katika sekta mbalimbali.

“Hebu fikiria, mtu aambiwe kwamba hawezi kuishi zaidi ya miaka 18, hali hiyo ni unyanyapaa na humnyima hamasa za maisha, atakosa bidii ya masomo na mambo mengine ya kimaisha.

Ni muhimu jamii iache unyanyapaa,” alisema Soka. Nchini kuna wastani wa wagonjwa 300,000 wa selimundu na huduma za vipimo vya utambuzi zipo katika hospitali kubwa tu kama Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bugando, Dodoma na nyingine kama hizo.

KATIKA kipindi cha miezi michache iliypopita, dunia ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi