loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Menina awaasa vijana kufanya kazi

MWIGIZAJI na mwanamuziki wa kike Menina Atiki amewahimiza vijana kufanya kazi kumsaidia Rais John Magufuli kulijenga taifa.

Akizungumza Dar es Salaamjana,  nyota huyo alisema kwa kutambua na umuhimu wa kazi yeye amekuwa akipambana kushiriki siyo tu katika uigizaji wa tamthilia bali kufanya biashara zinazomuingizia fedha.

“Sitegemei uigizaji peke yake nina mambo mengi nafanya, sisi kama vijana lazima tufanye kazi kwa bidii kumsaidia Rais Magufuli katika kujenga taifa,” alisema.

Menina alisema maisha ya sasa kama mtu hana mipango yanakuwa magumu hivyo ni muhimu kupangilia muda wa kila shughuli ili kuingiza fedha.

Msanii huyo ambaye aliibuliwa na shindano la kusaka vipaji (BSS) ambalo lilimtambulisha baada ya kuonekana na kipaji cha kuimba, licha ya kuwa sauti nzuri bado hajaweza kuitumia vyema kwani hajatoa nyimbo nyingi zaidi ameegemea katika uigizaji na biashara.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 15 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 15 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...