loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fainali ya Gofu CDF kuchezwa leo

MAMBO yamezidi kunoga katika michuano ya wazi ya Gofu iliyoandaliwa na klabu ya Lugalo baada ya wachezaji Nuru Mollel na Aidan Nziku kutangulia fainali na leo mchana atatafutwa bingwa kwa upande wa wachezaji wa kulipwa.

Aidha, wachezaji wa ridhaa zaidi ya 150 Jana walichuana vikali katika michuano hiyo ya Mkuu wa Majeshi (CDF) iliyodhaminiwa na benki ya NMB  kutafuta washindi ambapo baadhi yao walidai kuna upinzani hivyo wanahitaji kupambana zaidi kupata ushindi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa habari wa klabu ya Gofu Lugalo, Selemani Semunyu alisema viwango vya wachezaji vimekuwa bora kadiri wanavyokutana na upinzani hivyo, anaamini fainali hiyo itakuwa nzuri na yenye kuvutia.

"Mashindano yamekuwa ni mazuri mno,  mwamko umekuwa ni mkubwa, wachezaji wameonesha ubora na viwango vikubwa na kutoa changamoto kwa wengine kujitahidi," alisema Semunyu ambaye pia alishiriki katika michuano hiyo.

Baadhi ya wachezaji Maryanne Mugo alisema mashindano ni mazuri na kuwapongeza NMB na Lugalo kwa kuyafanya kuwa ya kuvutia kwani yamewapa hamasa ya kujituma kutokana na maandalizi mazuri.

Theonasi Thadei alisema kumekuwa na ushindani kwa sababu wamekutana na wachezaji wazuri ila kwa upande wake anafurahia ingawa anakiri kuna mahali alipata ugumu hasa katika sehemu ya umaliziaji kwani ni kama kulikuwa na mtego kidogo.

Patrick Karimi wa klabu ya Gymkhana alisema mchezo ulikuwa nzuri  na amevutiwa na uwanja ila yeye akikiri sehemu ya umaliziaji haikuwa nyepesi lakini alipambana kwa uwezo wake kumaliza mzunguko wa kwanza wa mashimo tisa.

Sherida Chilipachi wa klabu ya Gofu Morogoro alisema kwa zaidi ya miaka 27 amekuwa akishiriki mashindano tofauti hivyo, ushiriki wake msimu huu anaamini atamaliza vizuri na kuondoka na vikombe.

Alisema kwa idadi ya washiriki wakiojitokeza kwa atakayeibuka bingwa atakuwa ni mwenye kiwango kikubwa kwani upinzani ni mkubwa huku akiwashukuru Mkuu wa Majeshi nchini kwa kuandaa mashindano makubwa kama hayo yanayowakutanisha na marafiki wapya.

 

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 14 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 14 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...