loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NEC yamaliza hukumu pingamizi, ZEC yaengua 15

TUME  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wagombea 20 wa ubunge, wamepita bila kupingwa

Imesema awali ya wagombea walioteuliwa kama wagombea pekee, walikuwa 18, lakini sasa wamefikia idadi hiyo.

Aidha, NEC imerejesha wagombea watatu waliokuwa wameenguliwa awali katika majimbo ya Namtumbo, Bukene na Kavuu.

Taarifa iliyotolewa kwa umma Alhamisi wiki hii na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Wilson Mahera ilieleza kuwa baada ya kupitia na kuamua rufaa mbalimbali, tume hiyo imekubali rufaa tatu za kuwaengua wagombea wa ubunge katika majimbo matatu ; na imepokea taarifa ya kujitoa kwa wagombea katika majimbo ya Madaba mkoani Ruvuma na Chalinze mkoani Pwani na kufanya kuwe na wagombea pekee waliopita bila kupingwa.

Taarifa hiyo ilisema hadi kufikia  Septemba 17 mwaka huu, NEC ilipokea rufaa 616 zikiwamo 160 za ubunge, 456 za udiwani, malalamiko 25 na rufaa zilizojirudia 44.

“Kufuatia kumalizika kwa kipindi cha pingamizi na rufaa, wagombea waliopita bila kupingwa kwa mujibu wa Kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ni 20. Tume itawatangaza katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa sheria,”  alisema Dk Mahera katika taarifa hiyo. Alisema pia kuwa wahusika wamefikishiwa taarifa kwa utaratibu uliopo.

 “Baada ya kupitia rufaa zilizowasilishwa kutoka katika majimbo hayo, imerejesha wagombea watatu waliokuwa wameenguliwa. Hivyo basi majimbo hayo yataendelea na kampeni na uchaguzi utafanyika Oktoba 28, 2020,” alisema.

Dk Mahera katika taarifa hiyo alisema katika rufaa 160 za ubunge zilizoamuliwa na tume, wagombea waliorejeshwa ni 66, ambao hawakurejeshwa ni 32, rufaa zilizokataliwa na kuomba kuenguliwa wagombea ni 57 na zilizojirudia ni tano.

Alisema tume pia imepokea taarifa ya kujitoa kwa wagombea wa ubunge kwenye majimbo ya Chalinze na Madaba na hivyo kubakia wagombea pekee ambao wanakuwa wamepita bila kupingwa.

Katika hatua nyingine, 

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewaengua wagombea 15 wa nafasi ya Uwakilishi Zanzibar.

Wagombea walioenguliwa na idadi yao katika mabano ni wa Chama Cha ACT-Wazalendo (11), Chama Cha Mapinduzi  (1), Chama Cha Wananchi-CUF(1) , UPDP(1) na Demokrasia Makini (1).

Kwa mujibu wa ZEC, sababu za kuondolewa ni kushindwa kufuata kanuni za uchaguzi katika kujaza fomu za uteuzi.

Majina ya wagombea waliongeliwa ni ACT-Wazalendo, majimbo yao kwenye mabano ni: Haji Ali Haji (Tumbatu), Hassan Jani Masoud (Nungwi), Haji Mwadini Makame (Kijini), Juma Duni Haji (Mtoni), Hasne Abdallah Abeid (Bububu), Hamad Masoud Hamad (Ole), Omar Ali Shehe (Chake Chake), Khamis Rashid Khamis (Chonga), Issa Said Juma (Micheweni/Konde), Mmanga Mohammed Hemed (Konde/Tumbe) na  Is-haka Ismail Shariff (Wete).

Kutoka CUF ni Juma Ali Juma (Ole), Demokrasia Makini ni Abbas Omar Abbas (Ole),UPDP ni  Yussuf Said Hamad (Chake Chake) na CCM ni Othman Ali Khamis (Mtambwe).

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi