loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vyama 4 vyasitisha kampeni kwa ukata

WAKATI kampeni zikiendelea , vyama vinne vimesitisha mikutano yake ya kampeni kutokana na kile kilichoelezwa ni kukumbwa na ukata.

Vyama vilivyositisha mikutano ni NCCR-Mageuzi, Alliance for African Farmers (AAFP), Sauti ya Umma (SAU) na Democratic Party (DP).

Chama cha Wananchi ( CUF) kimebadili ratiba ambapo mgombea wake wa Urais, Profesa Ibrahim Lipumba atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni Pemba leo.

Ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inaonesha kuwa leo, wagombea wa kiti cha urais 17 na makamu (wagombea wenza) wangeendelea kunguruma katika maeneo mbalimbali nchini, lakini baadhi vimesitisha kampeni.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa vyama hivyo walisema wamelazimika ama kubadilisha ratiba au kusitisha mikutano kutokana na kushindwa kujipanga vizuri, huku vingine vikisema vinatafuta fedha.

Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR Mageuzi, Martin Mng'ong'o alisema wamesitisha kwa muda kampeni za mgombea urais na wakiendelea wataujulisha umma.

Mwenyekiti wa SAU, Bertha Mpata alisema chama chake kinafanya minada ya kuuza ng'ombe mikoani, kukusanya fedha na kuendelea na kampeni, lakini kwa sasa wamesitisha.

Katibu Mkuu AAFP, Rashid Rai alisema hawana uwezo wa kuomba, hivyo wanakusanya nguvu ya fedha kwanza wakifanikiwa wataendelea. Alisema kutokana na hilo, idadi ya mikutano yao itapungua

"Hatuna wa kumlaumu, sisi wenyewe hatukujipanga vizuri na hatuna uwezo na sasa tunakusanya nguvu kifedha," alisema Rai. AAFP walipaswa kuwa na mkutano wilayani Temeke, Dar es Salaam na kesho Kilosa mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa DP ambaye pia ni mgombea urais, Philipo Fumbo alisema wanapanga upya ratiba na marekebisho yatakuwa tayari Septemba 30 . Hata hivyo alisema  hana fedha za kwenda kila mahali.

Alisema ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa Rais, atatoa ruzuku kwa kila chama chenye usajili wa kudumu bila kujali kina mbunge au la.

CUF kwa upande wake, Katibu Mkuu wake, Haroud Mohamed Shamis, alisema  wamesitisha ratiba ya kampeni za mgombea urais, Profesa Ibrahim Lipumba mkoani Kigoma leo ili awe mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za urais wa Zanzibar zitakazofanyika leo Chakechake, Pemba. 

Katika hatua nyingine, ratiba ya NEC inaonesha mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli leo na kesho ataendelea na kampeni katika wilaya tatu za mkoa wa Tabora ambazo ni Uyui na Nzega na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan leo atakuwa wilayani Njombe mkoani Njombe.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu leo anatarajiwa kuwa mkoani Kigoma katika wilaya za Uvinza, Kibondo na Kakonko kabla ya kwenda wilayani Ngara mkoani Kagera.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi