loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais wa Burundi amsifu JPM kuibadili Tanzania

RAIS wa Burundi, Évariste Ndayishimiye amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanyia Tanzania; na kusema endapo wananchi wa Burundi wangekuwa Watanzania, wangempigia kura.

Aidha, ameshukuru na kuiita Tanzania mzazi kutokana na kuwa mstari wa mbele kusaidia Burundi, kila inapokumbwa na machafuko, lakini pia kupokea wakimbizi na kuishi nao kindugu.

Alisema nchi hiyo imetambua mchango wa viongozi wa Tanzania katika kujenga amani ya Burundi wakiwamo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Benjamin Mkapa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Rais Magufuli.

Rais Ndayishimiye alisema hayo jana wakati wa ziara yake ya kikazi nchini na kushiriki uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma.

“Nikupongeze sana kwa sababu umejenga Tanzania, umeibadilisha sana, mimi si mara yangu kwanza kuja hapa Tanzania, nimekuwa nakuja sana hapa Kigoma mimi na familia yangu, lakini kwa muda mchache tu nimekuja hapa nimeona mabadiliko,” alisema.

Alisema ana uhakika kwamba Rais Magufuli kwa watanzania ni baba yao, hivyo katika uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba mwaka huu, ushindi kwake ni lazima. “Warundi wote wanasema kama wangekuwepo hapa Tanzania wangemchagua Dk Magufuli,” alisema.

Alisema “Zamani Watanzania wakiona Mburundi anakuja hapa Tanzania walikuwa wanadhani kuna mambo mabaya Burundi, lakini sasa hivi nimekuja na salamu za wana Burundi wote wanawasalimia sana. Kwa niaba yao nataka nikupongeze kwa kuijenga Tanzania, umebadilisha Tanzania, nilikuwa nakuja hapa Kigoma, nimeona pamebadilika, nimeshangaa sana,” alisema.

Aliendelea, “Tunasema watanzania ni wazazi kwa sababu tangu zamani katika kupigania uhuru Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa anaenda bega kwa bega na viongozi wa Burundi. Wakati wa machafuko ya Burundi Tanzania ilikubali kubeba msalaba wa Burundi na kubeba wakimbizi.”

Alisema iliwaonea huruma Warundi na kufikia hatua ya kuwapa uraia wakimbizi waliokaa makambini kwa muda mrefu.

“Mimi ni rais lakini nakuona mheshimiwa rais (Rais Magufuli) kama baba yangu. Ndio maana nilisoma hapa ili nijue nitafanya nini, tulipata mambo mabaya kule Burundi, tulipompoteza baba yetu Nkurunziza (Pierre), mlikuwa nasi bega kwa bega. Asanteni sana,” alisema.

Alisema baba wa taifa ndiye alikuwa msuluhishi wa kwanza, baadaye akiwa kwenye mazungumzo ya amani alimfahamu kwa mara ya kwanza Rais mstaafu Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje. “Ndiyo sababu mtaona tunafahamiana sana, amekuwa kama baba yangu kwa sababu amenifundisha mengi,” alisema.

Rais huyo wa Burundi alisema mwaka 2015 wakati wa majaribio ya kupindua Burundi, Rais Mkapa ndiye alisaidia kwenye mazungumzo ya amani na kuwezesha waliokimbilia nje warudi, ikaandaliwa Katiba mpya iliyopitishwa na raia wa Burundi na kuirejesha nchi hiyo kwenye demokrasia.

Alisisitiza kuwa nchi yake iko tayari kufanya biashara na Tanzania, kwa kuwa kwa sasa hali ya usalama ni shwari .

Rais Magufuli alimshukuru Rais huyo kwa kuipa heshima Tanzania na kuwa nchi ya kwanza kuitembelea, baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Burundi hivi karibuni.

“Asante sana kwa hehima uliyotupa. Tunatambua Tanzania ni rafiki wa kweli wa Burundi.  Warundi na Watanzania waanze kuangalia mwelekeo mpya wa kujiona wao ni ndugu na wako ndani ya Afrika Mashariki,” alisema.

Aliahidi kushirikiana na nchi hiyo kwa hali mali katika nyanja zote za kibiashara, kisiasa, ulinzi na usalama na kijamii.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi