loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea CCM aahidi kujenga shule

MGOMBEA wa ubunge jimbo la Ilemela jijini Mwanza  kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Shibula kuwa atawajengea shule moja ya msingi na shule moja ya sekondari katika kata yao.

Dk Mabula alisema hayo wakati alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mhonze. Alisema kata ya Shibula ina shule moja tu ya sekondari inayoitwa Shibula na katika kata hiyo anatambua kuwa hakuna shule ya msingi hivyo atajenga pia na shule moja ya msingi.

Alisema ametenga shilingi milioni 55 kwajili ya ujenzi wa madarasa matatu na vyoo 10 katika shule ya sekondari Shibula.

Dk Mabula aliahidi kuwa ataweka barabara ya Lami pamoja na taa katika barabara ya Nyambuge kuelekea Shibula ambayo ina urefu wa kilomita 47.

Alisema Serikali imetenga shilingi milioni 612/- kwajili ya ujenzi wa Barbara za Bukala-Ilalila,Kahama-Igombe na Igogo kwenda Kabusungu.

 Mmoja ya watia nia ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Kafiti Kafiti aliwaomba wakazi wa Shibula wamchague  Dk Mabula na Swila Dede kwa upande wa udiwani. Kafiti alisema wananchi waendelee kuiamini Serikali ina mambo mengi mazuri ya maendeleo.

Mgombea udiwani wa kata ya Shibula kupitia CCM,Swilla Dede alisema Halmashauri itawasaidia wakazi wa Shibula katika utatuzi wa kero ya Maji na Umeme.

 Alisema walifanikiwa kupima ardhi katika mitaa yote 13 ya kata yao na aliomba wawekewe barabara ya lami katika njia ya Buswelu kuelekea Kayenze.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi