loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yabariki shughuli zote za Global Education Link

SERIKALI imesema inaunga mkono shughuli zote zinazofanywa na Global Education Link (GEL), na itaendelea kushirikiana nayo kwani imeonesha uzalendo wa hali ya juu katika kuisaidia Tanzania kupata wataalamu wa fani mbalimbali.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo wakati wa mahafali ya pili ya wanafunzi waliosoma nje ya nchi yaliyoandaliwa na (GEL).

Waziri Jafo aliipongeza GEL kwa namna ambavyo imekuwa ikifuatilia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi hao kuhakikisha wanahitimu, tena kwa viwango vinavyokubalika kimataifa.

Alisema GEL imekuwa ikiwasaidia wazazi wanaowekeza fedha nyingi kusomesha watoto wao nje ya nchi kuhakikisha thamani ya fedha zao inaonekana kwa kuhakikisha mwanafunzi hao wanahitimu kwa viwango bora.

“Kama kuna watanzania wazalendo basi wewe Abdulmalik(Mkurugenzi wa GEL) ni mzalendo sana, wewe na timu yako mnafanya kazi kubwa na nzuri sana, mnalisaidia taifa hili kusonga mbele kwa sababu vyuo tulivyonavyo na fani hatutoshelezi inabidi twende kusoma na nje pia mmeweka utaratibu mzuri sana,” alisema Jafo.

Waziri alimshauri Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalik Mollel kuanzisha siku maalumu ya GEL ambapo atakuwa akiueleza umma kuhusu fursa za wataalamu waliopo na wanaotarajiwa kupatikana kupitia taasisi hiyo.

 

Jafo alisema siku hiyo zialikwe kampuni, taasisi za fedha, taasisi za umma na binafsi kuelezwa kuhusu wahitimu wa fani mbalimbali na uwezo walionao ili kuwatengenezea milango ya ajira kwa waajiri hao.

Alisema hata wakati wa janga la virusi vya corona  GEL ilionesha uzalendo kwani ndiyo ilifanikisha kuandaliwa kwa masomo mtandaoni ambayo yalikuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wakati wote.

“Wakati ule tulitafakari tukaona tumtafute Mollel na alikubali na kuandaaa vipindi karibu 800 vya masomo kwenye Televisheni,  wazazi walikuwa wanaona tu kwenye televisheni lakini hawajui vinatokea wapi, kumbe ni kazi iliyokuwa ikifanywa na GEL,”alisema.

Pia Mollel na taasisi yake wakati huo wa virusi vya corona walionesha uzalendo mkubwa wa kuhakikisha wanafunzi wa Tanzania waliokwama nchi za nje wanapata usafiri wa kurudi nyumbani.

“Wakati ule wazazi walihamaki sana lakini uliwatuliza wakati unaandaa utaratibu na kweli ulifanikisha watoto wetu kurudi nyumbani salama, ingekuwa mtu mwingine angeweza kuwatelekeza lakini wewe hukuwaacha, hongera sana,” alisema

Kwa upande wake,  Mollel aliishukuru serikali kwa ushirikiano inaompa katika kutekeleza majukumu yake na aliahidi kuwa ataendelea kufuatilia mwenendo wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje.

Alisema mbali na kuwapeleka litakuwa jukumu lake kuhakikisha wanaporudi nyumbani wanaunganishwa na waajiri ili ujuzi walioupata uwe na manufaa kwa nchi yao.

“Kuanzia sasa jukumu la kuwapeleka wanafunzi nje ya nchi nawaachia wasaidizi wangu, mimi nataka nijikite kwenye kuhakikisha hawa wahitimu wanafanya nini baada ya kurudi. Tuna wahitimu wenye hadhi ya hali ya juu ambao wako tayari kufanya kazi waliyosomea kwa ubora,” alisema.

Waziri Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi