loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ni miaka zaidi ya 20 ya mafanikio MultiChoice Tanzania

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania imebainisha mambo makubwa iliyoyafanya hapa nchini tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka 20 iliyopita ikiwemo kutoa ajira, kukuza tasnia ya filamu na Sanaa huku ikiendelea kuwa kitovu cha burudani kitaifa na kimataifa kwa wateja wake wa DStv.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso wakati wa hafla maalumu ya wadau wa MultiChoice Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), mkurugenzi huyo alisema MultiChoice imekuwa kinara wa mapinduzi ya burudani hapa nchini kwa kuhakikisha kuwa inaongeza maudhui mengi ya ndani na pia kusaidia kuimarisha tasnia ya filamu hapa nchini.

“Miaka minne iliyopita, MultiChoice ilianzisha chaneli maalum ya Maisha Magic Bongo ambayo ni mahsusi kwa maudhui ya ndani. Chaneli hii inabeba maudhui ya kitanzania kwa asilimia 98 na maudhui haya huzalishwa hapa nchini na wazalishaji na waigizaji wa hapa nchini. Katika kipindi kifupi cha miaka minne, chaneli hii imetumia fedha nyingi kwa uzalishaji na ununuzi wa maudhui ya kitanzania na imefanya kazi na wazalishaji zaidi ya 200, waigiaji zaidi ya 2,000 na zaidi ya wasaidizi 5,000” alisema Jacqueline.

Katika kuimarisha tasnia ya filamu, Mkurugenzi huyo alisema kuwa kampuni hiyo inashirikiana na bodi ya filamu katika kutoa mafuzo kwa wazalishaji hapa nchini ambapo mwaka 2018 walifanya mafunzo katika mikoa mbalimbali na sasa wapo kwenye mazungumzo ya kushirikiana na bodi ya filamu kuendesha mafunzo maalum..

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau mbalimbali waliipongeza kampuni hiyo kwa jitihada zake za kutoa huduma bora na pia mchango wake katika tasnia mbalimbali hususan habari, michezo, burudani Sanaa na utamaduni.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dk Kiagho Kilonzo alisema kuwa wamekuwa na ushirikiano mkubwa wenye tija kati yao na kampuni hiyo na kwamba ushirikiano huo umezaa matunda kwa kusaidia katika kutoa ajira kwa wasanii kwa kununua kazi zao na pia kwa mafunzo mbalimbali.

Kwa upande wao, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie hapa nchini wamesema kuwa MultiChoice kupitia DStv imekuwa mkombozi mkubwa kwao kwani wamekuwa wakichukua kazi nyingi za wasanii wa ndani na hivyo kuwawezesha kiuchumi na kitaaluma pia.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Yanga bado sana- Kaze

masaa 14 yaliyopita Alexander Sanga,Mwanza

KOCHA Mkuu ...

Simba mwaka wa shetani

masaa 14 yaliyopita Mohamed Akida

MABINGWA wa ...

Yanga utaipenda tu

siku 1 iliyopita Alexander Sanga, Mwanza

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...