loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki, ushirika wakubaliana kuhusu uzalishaji kahawa

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Chama cha Kikuu cha Ushirika cha Ngara (NFCS-LTD) wamekubaliana kuendelea kushirikiana ili kuinua uzalishaji wa kahawa na kukuza pato la wakulima wa zao hilo katika wilayani Ngara.

Taarifa iliyotolewa jana na kumnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Justine Japhet  ilisema baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa chama hicho na  na TADB, pande zote zimetambua haja ya kuendeleza ushirikiano ili kuinua uzalishaji wa kahawa  na kuinua pato la wakulima wadogo wa zao hilo.

Viongozi wa chama hicho walikieleza kikao cha pamoja kuwa, changamoto wanazokumbana nazo watendaji wa ushirika ni pamoja na kutokuwa na vyombo vya usafiri, hivyo kushindwa kuwafikia wakulima kwa urahisi.

Aidha, walisema wakulima hawana elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji wa kahawa hali inayosababishwa kuzalishwa kiasi kidogo cha kahawa ikilinganishwa na mahitaji ya soko.

Benki hiyo iliahidi kutoa  pikipiki mbili kwa viongozi wa ushirika ili ziwawezeshe kuwafikia wakulima.

Ilisema  iko tayari kutuma Ngara wataalamu ili watoe elimu ya uoteshaji wa miche mipya ya mibuni ikiwa ni mbinu madhubuti  ya kuinua uzalishaji wa zao hilo.

Chama hicho cha ushirika kilianzishwa  mwaka 1993.  Hata hivyo, mwaka 2012 kilisitisha huduma zake kwa wakulima kutokana  nac hangamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa fedha ya kugharamia shughuli za chama na madeni ya kupindukia.

Mwaka 2018, TADB iliingilia kati na kukifufua chama hicho kwa kukitengenezea mfumo bora wa uendeshaji. 

“Chama kilipewa mkopo wenye riba nafuu uliokipa uwezo wa kukusanya kahawa hadi kufikia tani 2,300 kutoka kwa wakulima wadogo zaidi ya 500 wilayani Ngara,” ilieleza taarifa hiyo.

 

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Ngara

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi