loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafungwa zaidi ya 200 waambukizwa corona

WAFUNGWA zaidi ya 200 katika Gereza la Roumieh lililopo jijini Beirut, Lebanon wameambukizwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19.

Hata hivyo, taarifa  zilizotolewa na vyombo vya habari zilidai kuwa serikali ya nchi hiyo bado haijalipa uzito unaostahili suala hilo.

Taarifa hizo zilisema wafungwa wamekuwa wakilalamikia huduma mbovu za afya katika kukabili ugonjwa huo magerezani.

Gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 3,000. Linatajwa kuwa ni moja ya magereza yenye huduma mbovu nchini humo. Idadi hiyo ya wafungwa imezidi kiwango cha wafungwa kinachotakiwa kuwapo gerezani humo.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo wanashinikiza kuachiwa huru kwa wafungwa waliofanya makosa madogo, ili kupunguza mlundikano magerezani.

Lebanon ni kati ya nchi zenye  watu wengi walioathirika na covid-19.

Wakati huohuo, Serikali ya Uingereza imesema kuanzia Septemba 28, mwaka huu itaanza kutoza faini kuanzia euro 1,000 hadi 10,000 kwa wagonjwa wa covid- 19 watakaokaidi amri ya kujitenga.

Faini hiyo imelenga kuzuia watu hao wasisambaze ugonjwa huo kwa wengine.

Pia wakazi wa kipato cha chini, nao watapatiwa euro 500 kitakachowawezesha kumudu gharama za maisha wakati  watakapokuwa wamejitenga. Waajiri  watakaowafukuza kazi wagonjwa waliojitenga wameonywa kuwa watashtakiwa.

Taarifa iliyotolewa juzi, ilisema Uingereza ina maambukizi mapya 4,422 na vifo 27.

Akizungumzia faini hizo, Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, alisema zinalenga kuwabana watu wanaoshindwa kuendana na masharti yaliyowekwa.

“Uingereza imekuwa ikipuuzia masharti ya corona, ndio maana kwa sasa watakaokabainika kukiuka masharti watachukuliwa hatua kali ili makosa hayo yasijirudie,” alisema.

foto
Mwandishi: BEIRUT, Lebanon

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi