loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DCB yapongezwa kuwezesha Vicoba

SERIKALI imeipongeza Benki ya DCB na asasi ya Uyacode, kwa kuanzisha ushirikiano uliowezesha kuanzishwa miradi ya kilimo, ufugaji na viwanda vidogo kwa wanachama wa Vikundi vya Benki za Kijamii (Vicoba).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo katika kijiji cha Malivundo, wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani jana, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, alisema wanufaika wengi wa miradi hiyo ni wananchi wenye vipato vya chini na kati na kwamba vimewasaidia  kuwainua kiuchumi na kuchangia ukuaji wa uchumi.  

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa, Dk Kijaji alisema serikali imefanya maboresho mbalimbali kwenye sekta ya fedha, kutunga Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017.

Alisema kupitia Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019, kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha, Vicoba vilitambuliwa kama taasisi rasmi zinazoruhusiwa kutoa huduma ndogo za fedha kwa wanachama wake.

“Leo tukiwa tunazindua miradi hii ya kilimo cha kisasa, ufugaji wa kisasa na viwanda vidogo kwa wanachama wa Uyacode,  inaonesha jinsi gani asasi hii ilivyoweza kutumia fursa zilizopo kutokana na serikali yetu kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.”

“Nafahamu benki ya DCB inatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo, hivyo naamini wanachama wa Uyacode watanufaika na huduma hii kwa ajili ya kukuza mitaji yao kwa gharama nafuu na hatimaye kujikwamua kiuchumi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, alisema benki hiyo inatoa fursa zenye tija kwa wateja wake na kwa Watanzania kwa ujumla, ikijikita kutoa huduma na bidhaa za kimkakati zenye tija kwenye soko na zinazotoa wigo mpana kwa wateja wao.

Alisema kwa miaka kadhaa DCB imewekeza kwa kiasi kikubwa katika huduma zinazowalenga wajasiriamali walio katika vikundi na hivyo kubadilisha maisha ya na kukuza mitaji ya wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Uyacode, Michael Mgawe, alisema taasisi hiyo imekuwa ikipata mafanikia mbalimbali kwa kipindi cha miaka 18 hadi sasa.

“Pia tunatoa mikopo na kudhamini mikopo ya vikundi na wanavicoba, mikopo ya magari, bajaji, pikipiki, mashine za kusaga na kukobaa na pia kuweka mifumo mizuri ya makusanyo ya michango na marejesho ya mikopo katika vikundi vyao.

SEKTA binafsi kupitia wafanyabiashara wadogo na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Chalinze

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi